Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
Maalim Seif alisema hayo alipokuwa akizungumza na wajumbe kutoka
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar, waliofanya naye
mazungumzo huko nyumbani kwake Mbweni mjini Unguja, kuhusiana na
shughuli wanazozifanya.
Alisema mbinu muafaka ya kutokomeza vitendo hivyo ni kufanyika
utafiti wa kina ili baadaye wadu wote wakiwemo polisi, mahakama,
viongozi wa dini, wana jamii na serikali kuwekewa mkakati maalum katika
kufanikisha wajibu wa kila upande.
Maalim Seif alisema hali ya udhalilishwaji wanawake na watoto
Zanzibar imefikia katika kiwango cha kutisha na ni lazima hatua
zinazochukuliwa na taasisi mbali mbali, kikiwamo Chama cha Wanahabari
Wanawake (Tamwa), Zanzibar ziungwe mkono.
Alikipongeza chama hicho Zanzibar kutokana na kazi nzuri ya
kupigiwa mfano kwa kuelimisha jamii kukomesha vitendo vya udhalilishwaji
wanawwake na watoto.
“Kuishawishi jamii na hasa wanaume waachane na vitendo hivi si kazi
rahisi, lakini nyinyi mnaifanya kwa ufanisi, nadhani hatua mliyofikia
sasa ni ya mafanikio makubwa,” alisema Maalim Seif.
Mratibu wa Tamwa Zanzibar, Mzuri Issa, alisema mbali na kupiga vita
vitendo vya udhalilishwaji, Jumuiya hiyo inaendelea na juhudi za
kuwajengea uwezo wanawake wa Zanzibar katika maeneo tafauti, ikiwemo
kuwawezesha kushika nafasi za maamuzi, ikiwemo Ubunge na Uwakilishi.
Alisema mbali na wanawake kuonesha uwezo mkubwa katika kusimamia
majukumu, wapo wanaoshika nyadhifa mbali mbali, lakini wamekuwa
wakipambana na vikwazo vigumu wanapoamua kuwania nafasi za kisiasa
kupitia vyama.
No comments:
Post a Comment