Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda zaidi ya 50 wa jijini Dar
es Salaam wameandamana hadi katika ofisi za gazeti hili kulalamikia
unyanyasaji wanaofanyiwa na polisi jamii.
Bodaboda hao kutoka maeneo ya Tanki bovu, Kawe na Mwenge wanadai
kuwa wamechoshwa na unyanyasaji wanaofanyiwa na polisi jamii ambao
wamekuwa wakiwakamata ovyo katika maeneo mbalimbali ya Jiji.
Kalos Meltus, alisema wamekuwa wakikamatwa na kutozwa faini kati ya
Sh. 30,000 na 100,00 kila wanapoingia katikati ya Jiji na kudai kuwa
wamegeuzwa mtaji wa baadhi ya viongozi kujipatia pesa.
Naye Erasto Matheo, alisema kuwakamata bodaboda katikati ya Jiji
kunawaathiri kiuchumi kwa sababu wateja wao wengi wanakwenda mjini hivyo
kuendelea kuwazuia ni kuwapa wakati mgumu kimaisha.
No comments:
Post a Comment