Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema.
Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya elimu, Mjema alisema
anasikitishwa na baadhi ya wazazi wanaokwepa majukumu yao kwa kuwaruhusu
watoto wao kushiriki katika vitendo hivyo na kusababisha elimu
kuporomoka.
Hata hivyo, aliwapongeza watendaji na wadau wa elimu kwa jitihada
zao za kuisaidia wilaya hiyo hadi mwaka huu kuwa ya kwanza mkoa wa Dar
es Salaam kwa kufaulisha wanafunzi zaidi ya asilimia 70 .
Maadhimisho hayo yaliyofanyika Kata ya Kijichi yaliandaliwa pamoja
na Manispaa Temeke, taasisi ya kijamii ya Ocode na Shirika la Kimataifa
la We World ambapo baadhi ya shule na wanafunzi waliofanya vizuri
walipewa zawadi.
“Haiwezekani mtoto anatoka masaa matatu bila taarifa halafu mnakuwa
kimya, muda huo ni mwingi kwa binti kuharibu maisha yake, ngoma za
vigodoro na safari za ufukweni si salama lazima tuhakikishe tunawajibika
kuwakemea,” alisema Mjema.
Alisema mwaka huu waliamua kufanya kazi maalum kwa ajili ya kuinua
kiwango cha elimu ambapo matunda yake yameonekana baada ya ufaulu
kuongezeka kwa shule za msingi na sekondari.
Alisema ufaulu kwa shule za msingi ulikuwa asilimia 72 mwaka jana
kutoka asilimia 60 mwaka 2003 na asilimia 64 kutoka chini ya asilimia 50
kwa sekondari.
“Ufaulu huu umeonyesha jinsi tulivyoamua kuwa pamoja kati ya
serikali na wadau kuhakikisha elimu yetu inakua kwa kasi, nawapongeza na
nawataka kuongeza kasi zaidi ili tuongoze ngazi ya Taifa,” alisema.
Mratibu wa Ocode, Joseph Jackson, alisema kwa kushirikiana na We
World wametumia jumla ya Sh. milioni 655.9 kwa ajili ya kuboresha
mazingira na utendaji wa kazi ya walimu kwa shule nne za msingi.
Alizitaja shule zilizonufaika kuwa ni Kijichi, Bwawani, Kibondemaji na Buza.
Alisema shule hizo zimeboreshwa kwa kukarabatiwa madarasa, mitandao
ya maji, jiko kwa ajili ya kupikia chakula cha wanafunzi pamoja na
ununuzi wa madawati kwa shule hizo.
No comments:
Post a Comment