Polisi
wamelazimika kufyatua risasi na mabomu ya kutoa machozi kwa
waandamanaji waliokaribia makao ya rais katika mji muu wa Bujumbura
Burundi.
Mwandishi wa BBC aliyeko huko Maud Jullien amesema kuwa
mamia ya waandamanaji walikuwa takriban kilomita moja kutoka kwa kasri
ya rais ndipo wakavamiwa na maafisa wa usalama.Hii ndio mara ya kwanza kwa waandamanji hao kukaribia kasri ya rais mjini Bujumbura tangu maelfu ya watu kuanza kuandamana kupinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kuwania kuingoza taifa hilo kwa awamu ya tatu kinyume na mwafaka wa amani wa Arusha.
Viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki na kati wanakutana hii leo mjini Dar es Salaam kujadili mbinu za kutatua mgogoro wa kisiasa ambao inalaumiwa kwa kusababisha vifo vya watu 20.
Mkutano huo utakuwa chini ya uenyekiti wa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, aliyeuitisha baada ya ujumbe wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Jumuiya hiyo, kwenda Bujumbura wiki iliyopita.
Rais Pierre Nkurunziza ambaye analaumiwa kugombea urais kwa muhula wa tatu, anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo,kusikiliza hoja za viongozi wenzake.
Viongozi hao wanatarajiwa kumshinikiza rais Nkurunzinza kuahirisha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi juni.
No comments:
Post a Comment