Dar es Salaam. Katika dakika za mwishomwisho wakati wa mchakato wa kuwania urais kwa tiketi ya CCM, habari za mmoja wa wagombea aliyekuwa na nguvu katika kinyang’anyiro hicho, Edward Lowassa kwamba angeenguliwa zilivuma mno na kuibua swali la atakatwa hakatwi?
Tuesday, 4 August 2015
Wednesday, 29 July 2015
Dk. Benson Bana.
MAKAMU RAIS TEC
Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Mhashamu Severine Niwemugizi, alisema hatua ya Lowassa ni ukomavu wa vyama vya siasa nchini hasa vya upinzani kuwa mtu yoyote anaweza kuhama na kujiunga na chama chochote.
Alisema kuhama kwa Lowassa kunatafsiri kuwa mchakato wa uteuzi ndani ya CCM haukumridhisha.
“Tafsiri ni kuwa ameona CCM haikumtendea haki na kama binadamu yeyote ana haki ya kuchukua hatua kama binadamu mwingine, mtu anapoona hajatendewa haki kama binadamu uamuzi ni wake kuondoka kama wengine wanavyobadilisha vyama, hatushangai ni jambo linatokea kwa wengi siyo la pekee sana,” alisema na kuongeza:
CCM yaonya vijana kubeza wagombea wake.
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Onyo hilo alilitoa juzi baada ya baadhi ya vijana hao kuwauliza maswali ya kejeli wagombea ubunge hao, wakati wakijinadi kwenye mikutano ya chama hicho katika kata za Mshangano, Msamala na Bombambili.
Marko alisema wagombea hao wanaomba ridhaa kwa wanaCCM ili apatikane mmoja wao wa kupeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini Oktoba 25, mwaka huu.
Alisema wanachama wa vyama vingine hawana ruhusa ya kuwauliza maswali wagombea wa CCM bali wasubiri atakapopatikana wa kupambana na atakayechaguliwa kutoka vyama vingine vya upinzani.
Vilevile katibu huyo amewataka wanachama wa chama hicho kuacha tabia za kuuliza maswali ya kupandikizwa wagombea hao bali wafanye hivyo kwa kwa utashi wao.
Wagombea hao ni Leonidas Gama (Mkuu wa mkoa Kirimanjaro), Francis Miti (Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ mkoani Arusha), Theresia Uvisa ambaye (alikuwa mbunge viti maalum kupitia vyuo vikuu vishiriki na Waziri wa Mazingira), Azizi Mohamed (Katibu wa CCM Namtumbo), Sebastian Waliyuba (Wakili wa kujitegemea).
Wengine ni Erick Mapunda (Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya) ,Raymond Mhenga (Ofisa Masoko wa Claus FM) na Mussa Gama ambaye ni mtoto wa Marehemu Lawrence Gama (Katibu Mstaafu wa CCM ).
Tuesday, 28 July 2015
“Watanzania wanataka mabadiliko...watayatafuta nje ya CCM"
Dar es Salaam. Kauli ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kuwa Watanzania wanataka mabadiliko na wasipoyapata ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM inaweza kutimia mwaka huu.
Lowassa sasa rasmi Ukawa,muda wowote kutangazwa mgombea urais
Lowassa aliondoka hotelini hapo baada ya kukaa kikaoni kwa saa 1.38 (dakika 98). Aliagwa na viongozi mbalimbali wa Chadema.
Thursday, 9 July 2015
Maoni juu ya Burundi: wakati wa kuchukua hatua ni sasa
Serikali ya Burundi imeshinda uchaguzi wa Bunge.Lakini uchaguzi huo ulikuwa hadaa. Siku chache kabla ya uchaguzi wa Rais nchini humo hatari ya kuzuka vita vingine vya wenyewe kwa wenyewe imezidi kuwa kubwa .
Matokeo ya uchaguzi wa Bunge nchini Burundi hayakumshangaza yeyote. Uchaguzi huo haukuwa huru wala wa haki. Kwani, ulifanyika bila ya usimamizi wa tume huru ya uchaguzi na bila ya waangalizi huru.
Vituo vitatu vya televisheni vyatozwa faini, vyaony
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Prof. John Nkoma.
Vituo hivyo ni Chanel Ten kupitia kipindi chake cha Kanjanja Time kimepewa onyo na kutozwa faini ya Sh. milioni 2.5, Star Tv kupitia kipindi chake cha Min Buzz kimepewa onyo na faini ya Sh. 500, 000 na Tanzania Broadcasting Corporation (TBC1) onyo na faini ya Sh. 500, 000 kwenye mojawapo wa taarifa za habari zilizorushwa na kituo hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Margeret Munyangi, alisema wameamua kuchukua hatua hizo baada ya kamati hiyo kukaa na kujadili ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005.
Alisema Mei 30, mwaka huu, kituo cha Chanel Ten kupitia kipindi cha Kanjanja Time kilichorushwa hewani kuanzia saa 2:45 hadi saa 3:10 usiku taarifa iliyoonyesha picha ya mgonjwa akiwa katika wodi ya Hospitali ya Serikali mjini Songea huku sehemu ya makalio yake yakiwa wazi na kuonyesha vidonda.
Niyonzima: Nauguza, wakipona nitarudi.
Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha.
Akizungumza na gazeti hili juzi mchana kwa njia ya simu kutoka Kigali, Rwanda, Niyonzima alisema atarejea nchini mara tu hali ya watoto wake itakapokuwa vizuri.
Niyonzima alisema anafahamu majukumu yake ndani ya klabu na kinachomchelewesha kurejea nchini, ni kutekeleza majukumu yake kama baba wa familia.
"Nitarudi hivi karibuni Inshaallah, hivi tunavyoongea na wewe niko hospitali, nipigie baadaye tutaongea zaidi," alisema kwa kifupi Niyonzima alipozungumza na gazeti hili juzi Julai 7, mwaka huu saa 6:19 mchana kwa saa za Tanzania sawa na saa 5:19 kwa saa za Kigali, Rwanda.
Jana kiungo huyo hakuweza kupatikana tena katika simu yake ya mkononi inayoishia na namba ...719 kuelezea zaidi tatizo linalomchelewesha kurudi nchini kushiriki kwenye mazoezi pamoja na wachezaji wenzake.
Majina yao kuanikwa leo, wengine 33 kufyekwa.
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa mujibu wa habari kutoka mitandao ya kijamii, kwenye vijiwe na mijadala sehemu mbalimbali, majina hayo matano yanaaminika kwamba yatatoka miongoni mwa watiania 10 ambao wametajwa zaidi katika mijadala hiyo.
Sababu kuu mbili ambazo zimekuwa zikitolewa kwenye mijadala hiyo na hata na baadhi ya wachambuzi wa mambo ya siasa Tanzania ni mbili. Mosi, uzoefu wao ndani ya ungozi wa serikali na pili, nafasi yao ndani ya chama, ama kama wajumbe wa NEC au Kamati Kuu.
Majina ambayo yanatazamiwa kwamba yanaweza kupenya Kamati Kuu ni pamoja na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal; Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe; Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro; Waziri Mkuu Mizengo Pinda; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya; Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani; Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli;.
Subscribe to:
Posts (Atom)
