ad

ad
Showing posts with label MAZINGIRA NA JAMII. Show all posts
Showing posts with label MAZINGIRA NA JAMII. Show all posts

Sunday, 8 January 2017

Uzinduzi wa Soko la matunda

soko-wete
  Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali mara alipowasili katika viwanja vya Soko la Matunda Wete leo katika Uzinduzi rasmi wa Soko hilo sambamba na Ofisi ya Baraza la Mji Wete, katika sherehe za shamara shamara za  Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapindzi Zanzibar.
soko-wete-1
Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali mara alipowasili katika viwanja vya Soko la Matunda Wete leo katika Uzinduzi rasmi wa Soko hilo sambamba na Ofisi ya Baraza la Mji Wete, katika sherehe za shamara shamara za  Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapindzi Zanzibar.
soko-wete-2
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana na Waziri wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe,Mohamed Aboud Mohamed alipowasili katika viwanja vya Soko la Matunda Wete leo katika Uzinduzi rasmi ,uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika sherehe za shamara shamara za  Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapindzi Zanzibar.
soko-wete-3
 Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata Utepe  kuashiria uzinduzi wa  Soko la Matunda   na Ofisi ya Baraza la Mji la Wete katika Shamara shamra za Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar,(kulia) Mke wa Rais  wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe.Omar Khamis Othman (wa pili kushoto).
soko-wete-4
 Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Nd,Radhiya Rashid wakati alipolitembelea Soko la Matunda Wete Mjini Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya kulizindua rasmi leo katika Shamara shamra za Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.
soko-wete-5
4399//// Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Nd,Radhiya Rashid wakati alipolitembelea Soko la Matunda Wete Mjini Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya kulizindua rasmi leo katika Shamara shamra za Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.
soko-wete-6
Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwapungia mkono Wananchi wa Wilaya ya Wete leo baada ya kulizindua rasmi Soko la Matunda na Ofisi ta Baraza la Mji Wete Mkoa wa Kaskazini ikiwa ni katika Shamara shamra za Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar,(katikati) Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Nd,Radhiya Rashid .
soko-wete-7Baadgi ya Wananchi waliohudhuria katika sherehe za Uzinduzi wa Soko la Matunda na Ofisi ya Baraza la Mji Wete Wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba ikiwa ni miongoni mwa Shamara shamara za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapindzi Zanzibar.
soko-wete-8
Baadgi ya Wananchi waliohudhuria katika sherehe za Uzinduzi wa Soko la Matunda na Ofisi ya Baraza la Mji Wete Wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba ikiwa ni miongoni mwa Shamara shamara za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapindzi Zanzibar.
soko-wete-9
Soko la Matunda Wete Wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba likiwa tayari kwa matumizi ambapo leo limezinduliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika sherehe za shamara shamara za  Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapindzi Zanzibar, [Picha na Ikulu.] 08Jan 2017.

Saturday, 30 April 2016

Kujuana Vizuri Kabla ya Kuanzisha Mahusiano


 

 Na Kalonga Kasati

Kumekuwa na imani potofu kwa wanawake kwamba Hawawezi kumwambia ukweli Mwanaume anampenda Kwanza Mpaka Mwanaume aanze lakini ukweli usiopingika ni Kwamba wao pia Hupendi na Mara nyingi wao Wakianza kupenda Hupenda kweli kufikia Stage Hata ya kuhisi kuumwa. Hizi ni dalili za Mwanamke anaekupenda ila anagoma kukwambia tu.
Hufanya mambo ambayo yatamfanya kuona kama Unampenda na kumthamini au la mfano wa Mambo hayo ni kama kujifanya anaumwa na kauangalia Respond yako kwake ni kiasi gani Unamjali na kiasi gani Utahangaika kwa ajili yake.

Kucheka kwa Nguvu Hata kwa kitu kisicho chekesha Endapo Wewe Umezungumza. Mara Nyingi Ataonesha Uso wa furaha Hata kama si furaha ya kweli


Hujisikia wivu anapokuona na Wasichana Wengine. Ukiwa unachart nao na Ukiwaita Majina Ya kimahaba. Hapendi na hupenda yale afanyiwe Yeye tu Hata kama Sio Mpenzi wako.

Anakumbuka siku zako Muhimu. Hukumbuka kama Vile siku yako ya kuzaliwa hatoweza kuisahau kufanya ipite Bila kukutakia heri ya Siku ya kuzaliwa kama sivyo Ukifaulu Mtihani Au chochote katika Maisha yako atakuwa Mbele kukupongeza.

Eye contact hupendelea sana kukuangalia machoni Muda Wote ambao Mtakuwa Mkizungumza pamoja akidhani kuwa utamuelewa ni kiasi Gani anakupenda kupitia vile Anavyokuangalia. Ila Wengine Huona aibu kuwatazama Wavulana Wanaowapenda hivyo Huweka Jicho la wizi na kukuvizia.

Hupenda kukaa muda mwingi na wewe. Hawezi kupoteza Hata Sekunde Ukimuhitaji kwa Mazungumzo. Anajisikia furaha kukaa na Wewe Muda Mrefu bila kuchoka. Anaweza akaacha Kila kitu anachokifanya ili ajumuike na Wewe na akikaa na Wewe hupendelea Sana Mwanzoni Kukujua Wewe Zaidi na Hukujengea Mazingira ya Wewe Uwemuwazi ili Umwambie Mengi kuhusu Wewe na pia akiwa na Wewe atakuwa Muwazi zaidi Hadi Mavazi aliyovaa Hupenda Sana kujua Yako na kukuambia yake na Hupenda kujua ni Mavazi Gani Yeye akivaa Anakuvutia zaidi Na atajitahidi kuwa anavaa ya style hiyo kukufurahisha.

Kama Msichana anakupenda yupo Tayari kusacrifice. Ni kitu ambacho Hakuna mtu ambaye Anaweza akafanya kwa Mtu Mwingine. Utamuona Vipi huyo Msichana alivyo kwako na kwa Wengine. Yaani yupo Tayari akose lakini Wewe Upate na kwa Mwingine anaweza Akamwambia Hana alichoombwa lakini akakupa Wewe kama Pesa na vitu vingine.

Mikwaruzano ikitokea katika Urafiki wenu Hayupo tayari kukupoteza kabla hajakwambia Nakupenda.Kwa kuwa anakupenda endapo ikitokea mikwaruzano Basi atafanya Juu chini Kuyaweka Mambo sawa ili asikukose.

Mwanamke anaekupenda hupenda kujua Mengi sana kuhusu Wewe na hapo inamsaidia kukununulia Zawadi za Mitego kama Boxer , na Mara nyingi Hupenda Rangi Nyeupe, au kukununulia perfume , aSbuni ya kuoge ya Manukato,soksi, vest, bukta, Saa,raba, t-shirt. Na kama Mkitoka Wote Mkaenda Shopping ataakutega kwa kukuonyesha Vitu na Wewe Ukionekana Umependa kitu Hatonunua siku hiyo ila atanunua iSku inayofuata na kukuletea kama suprise.


Mwanamke anaekupenda ili akujue zaidi Hupendelea msosi mle Sehemu Mmoja na kama ikitokea Mwanaume Hawezi kuhama Sehemu anayokula Mwanamke Yupo Radhi kubadili na kumfuata Mwanaume Hata kama Sehemu hiyo yeye Haipendi na kama Unakula kwako Basi Atakutega na kuja kupika kwako ili Mle na atakuwa anapenda Kununua vitu vya kupika ili tu Akutekena Uone Upendo wake.

Ukiona Dalili kama Hizi Mwanaume Tafadhali Fanya Mpango wa kumweka ndani (oa) Mwanamke huyo kabla ujachelewa alafu Ukaja kuangukia kwa wale Wanawake Wenye sifa ya Mbaya

Thursday, 28 April 2016

Serikali kupata Maoni ya Wananchi Kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Ndoa na kutungwa kwa Sheria Mpya ya Mirathi na Urithi

 
 
 
 Na Mwandishi wetu

Serikali   imejiandaa kuleta Muswada wa Sheria bungeni kutoa haki ya kusoma kwa watoto wote wa kike na kiume wa shule za msingi, sekondari Na kutoruhusiwa kuoa au kuolewa.

Aidha, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema Serikali inaendelea kukamilisha utaratibu wa kupata maoni ya wananchi kuhusu marekebisho ya Sheria ya Ndoa na kutungwa kwa Sheria mpya ya Mirathi na Urithi kuondokana na mkanganyiko uliopo kuhusu sheria hiyo.

Bunge lilielezwa hayo jana mjini Dodoma wakati waziri huyo akijibu swali la Nyongeza la Mbunge wa Ileje, Janeth Mbene (CCM) aliyehoji ni lini serikali itaanza maandalizi ya kuchukua maoni juu ya kufanya marekebisho sheria ya ndoa ya mwaka 1971.

Akijibu swali hilo, Dk Mwakyembe alisema hatua za awali zimeshaanza kuchukuliwa na wizara hiyo ili kupata maoni ya wananchi juu ya Marekebisho ya sheria hiyo ya ndoa ya mwaka 1971 na kutungwa kwa sheria mpya ya mirathi na urithi.

Alisema serikali ina nia ya dhati ya kufanyia marekebisho sheria ya ndoa na kwamba mchakato huo ulisitishwa kwa kuwa Tume ya mabadiliko ya Katiba ilikuwa ikikusanya maoni kuhusu mabadiliko ya katiba , hivyo walidhani Wananchi wangetoa pia maoni juu ya sheria hiyo.

Thursday, 21 April 2016

Picha ya Mwanamke wa kwanza Marekani Kuwekwa Kwenye Dola

Marekani kuwaenzi watumwa.


Picha ya Mtumwa Mmoja aliyekata nyororo na kisha kusaidia Mamia ya Wenzake kutoroka Utumwa sasa itatumika katika Noti Mpya ya Dola 20 nchini Marekani.

Bi Harriet Tubman atakuwa Mwafrika Mmarekani wa kwanza kuangaziwa kwenye sarafu ya Marekani.

Vilevile ndiye Mwanamke wa kwanza katika kipindi cha karne moja katika Historia ya Marekani Picha yake kuwekwa kwenye Dola.

Picha hiyo itabadilishwa na ile ya awali ya Rais wa Saba wa Marekani Andrew Jackson Ambaye Alikuwa akimiliki Watumwa enzi hizo.

Sasa Picha ya Andrew Jackson itakuwa Nyuma ya noti hiyo.

Noti hiyo itaanza kutumika Mwaka 2020 lakini idara ya fedha nchini Marekani imesema ni Mwanzo wa kuwakumbuka na kuwaenzi waliopigania haki za kibinadamu nchini humo.

Bi Tubman alizaliwa miaka ya 1800 utumwani jimbo la Maryland. Alifariki 10 Machi, 1913 Akiwa eneo la Auburn, jimbo la New York.

Wednesday, 20 April 2016

Mwili ambao Ulikuwa Bado Umepatikana

Mnamo majira ya saa 10 alfajiri, gari aina ya Hiace  iliteleza toka kwenye kivuko na kutumbukia katika bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam.

Gari hiyo ilikuwa na abiria wawili. Mpaka majira ya asubuhi, jeshi la Zimamoto na uokoaji lilifanikiwa kuupata mwili mmoja na likaendelea kuutafuta mwili wa pili. 
 
Mchana  huu  umepatikana mwili wa pili  wa Nice Karagwe  huku zoezi la kuitoa gari likiendelea

Na Chrispino Mpinge

 Muonyeshe umempa akili yako na umakini kwa hali flani. Wanawake wanapenda sana Wakiwa wanaongea na mwanaume, na mwanaume huyo akawa anawapa umakini wa kuwasikiliza. Tofauti na hapo wanawake huwa wanaishiwa mvuto na mwanaume ambae Anawapa umakini kiasi cha kupitiliza, umakini huu sio wa kusikiliza bali ule wa kuonyesha Wewe ndo unaejua kupenda kwa kumpa sifa nyingi katika hali ambayo hazihitajiki

Najua huwa tunatumia muda  mwingi sana vijiweni tukiongelea, sehemu gani nzuri ya kukutana na wanawake, jinsi ya kuwatongoza na kuanzisha maongezi, nini cha kuongea na kufanya ili akuelewe na mrembo awe wako, Lakini hayo yote ambayo huwa tunayaongelea Huwa ni kama theluji kwenye mlima Kilimanjaro, ila volkano yenyewe huwa ni jinsi ya kuwafanya wanawake waanze kukuhangaikia na kukufuatilia, na hizi hapa ni njia tano za kuwa wapekee na kuwafanya watoto wenyewe wa kike wawe wanakuhangaikia.

Naomba nitilie mkazo jambo moja, njia hizi hakikisha hauzichukulii juu juu, zielewe na Zitunze vizuri kwenye akili yako, maana unahitaji kila kitu uwe umeshakielewa kwa yote Tuliozungumzia hapa kiumeni kuhusu wanawake.

Namba 1. Tengeneza mvuto unaovutia kwake mara ya kwanza unaongea nae.

Sifa ya mwanaume wa kweli huwa ni kujiamini, na mwanamke sikuzote anavutika na Mwanaume wa kweli, onyesha kujiamini na kuwa mkufunzi wa mchezo wa Kutongoza toka Moyoni bila hata kufikiria utaongea nini au kujishitukia, utaona mwanamke mwenyewe hata kama angekuwa amekutegea mgongo atageuka na kuanza kukusikiliza kwa mvuto, mkibadilishana namba kesho mwenyewe ndo atapiga simu na kuanza kujitambulisha, “Halo, mie ndo yule dada tuliobadilishana namba”, mwenyewe anaanza kujinogesha, kukufatilia na kukuwinda.

Namba 2. Muonyeshe changamoto.

Mwanamke akihisi wakati unamtongoza kuwa umeshakufa kwake ukaoza, huna mwingine yeye ndio yeye, unamuhitaji kupitiliza kwa hiyo utafanya chochote, moja kwa moja anakuweka kwenye kundi la FALA, (Samahani kwa kutumia kiswahili kibaya, ila ndo hivyo), mwanamke sikuzote huwa havutiki na mwanaume Fala, mwanaume ambaye mapenzi yanamuendesha.

Namba 3. Muulize maswali ya namna flani.

Mwanamke akishakusoma na kukuona wewe ni mwanaume wa aina flani, kuna uhakika Mkubwa ataendelea kukufikiria kuwa wewe ni mwanaume wa aina hiyo, kwa hivyo ukianza kuonyesha tokea mwanzo we ni mwanaume yule anaye lilia mapenzi, basi ataanza kukuona fala tokea mwanzo, mwanaume ambae utamfuata fuata hata pale ambapo hautakiwi, na Unajua wanawake wanahisia gani na wanaume wa aina hii. Kwahiyo ukianza na maswali Ya kuonyesha tabia ya kifala, patishia huyo mwanamke ataanza kukufikiria kuwa utakuwa na Tabia hizo hizo kwa kipindi chote cha maisha yako, na huo ndo utakuwa mwisho wako.

Namba 4. Usimfuatilie sana.

Usipoonana na mtu sana mara kwa mara hukufanya uanze kumkumbuka, na hii kanuni ukiitumia vizuri kwa mwanamke utamfanya aanze kukuulizia kwa rafiki zako, iwapo Ungeitumia hata kwa naniii hata hizo meseji ambazo hakujibu angekuwa anazijibu. Iwapo Ukiwa unapendelea kumuona ona huyo mwanamke, au husubiri na kumpa muda mwanamke kumpigia simu mara baada ya yeye kukupigia, utafanya siku zote uwe kwenye uhusiano wa Upande mmoja.

Namba 5. Muonyeshe umempa akili yako na umakini kwa hali flani. Wanawake wanapenda Sana wakiwa wanaongea na mwanaume, na mwanaume huyo akawa anawapa umakini wa kuwasikiliza. Tofauti na hapo wanawake huwa wanaishiwa mvuto na mwanaume ambae Anawapa umakini kiasi cha kupitiliza, umakini huu sio wa kusikiliza bali ule wa kuonyesha Wewe ndo unaejua kupenda kwa kumpa sifa nyingi katika hali ambayo hazihitajiki






Tuesday, 19 April 2016

Upigaji Marufuku Matumizi Ya Mifuko Ya Plastiki

Serikali imetaka Shule Binafsi Kuwa na Mihula Miwili ya Masomo

 

WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imeziagiza shule zote za binafsi kuwa na Mihula miwili tu ya masomo kwa mwaka badala ya kuwa na mihula mitatu au minne kama ilivyo kwa sasa katika shule hizo.

Agizo hilo liko kwenye Waraka wa Elimu Namba Moja wa Mwaka 2015, ambao unaeleza kuwa kuanzia sasa mihula ya masomo, itakuwa miwili kwa kila mwaka wa masomo kwa shule zote za Serikali na zisizo za Serikali.eustella-Bhalalusesa1

Waraka huo uliosainiwa na Kamishna wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa umefafanua kuwa kila muhula, utakuwa na likizo fupi na likizo ya mwisho wa muhula. Siku za masomo kwa mwaka zitakuwa ni 194.

Waraka huo pia umeagiza wanafunzi wote, wapumzike mwezi Juni na Desemba na Mashindano ya michezo ya shule za msingi (Umitashumta) na michezo ya sekondari (Umiseta), ifanyike mwezi Juni wakati wa likizo.

Kutokana na agizo hilo, wamiliki wa shule zisizo za serikali wametakiwa kuwasilisha wizara ya Elimu kalenda za mihula ya masomo. Nakala ya waraka huo wamesambaziwa wakaguzi wote Wa shule, walioko kwenye kanda na wilaya kuhakikisha wanazifuatilia shule zote ili ziweze kutii agizo hilo la Serikali.

Profesa Bhalusesa alifafanua katika waraka huo, umekazia Waraka wa Serikali Namba 5 wa Mwaka 2012 ambao ulikuwa unaelekeza mihula ya masomo kwa shule za sekondari na vyuo Vya ualimu, ifanane ili kuepusha usumbufu kwa walimu na kwa wanafunzi.

Friday, 15 August 2014

MAZINGIRA NA JAMII

MACHIMBO YA MADINI YA MCHANGA

MACHIMBO ya madini ya Ujenzi(Mchanga)ni bidhaa ambayo inalijenga Taifa letu, lakini kwa upande wa pili wa shilingi,uchimbaji wa madini hayo,unayaweka mazingira yetu katika hali hatarishi kwa vizazi vijavyo.
LORI aina ya Isuzu likitoka eneo la mgodi wa machimbo ya madini ya Ujenzi chimbo la