Friday 15 August 2014

MAZINGIRA NA JAMII

MACHIMBO YA MADINI YA MCHANGA

MACHIMBO ya madini ya Ujenzi(Mchanga)ni bidhaa ambayo inalijenga Taifa letu, lakini kwa upande wa pili wa shilingi,uchimbaji wa madini hayo,unayaweka mazingira yetu katika hali hatarishi kwa vizazi vijavyo.
LORI aina ya Isuzu likitoka eneo la mgodi wa machimbo ya madini ya Ujenzi chimbo la
Mwanadulatu,Mkuranga Mkoani Pwani.
UPAKIAJI wa madini ya ujenzi kataka malori ndio kazi kubwa kwa vijana wa mwanadulatu,wilaya ya Mkuranga ,Mkoa wa Pwani ,ambapoo kwa sasa Vijana hao wamejikita katika ajira hiyo.
SIO mlipuko wa Bomu ila ni vijana wapo kazini wakipakia Madini ya Ujenzi(Mchanga)Madini hayo yanapatikana katiaka kijiji cha Mwanadilatu kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani,kilomita 5 toka mbagala rangi tatu.
VIJANA wakieka sawa madini ya Ujenzi(Mchanga) waliyoyapakia katika gari,ambayo yapo tayari kwenda kufanyiwa ujenzi mbalimbali ndani na nje ya nchi,chimbo la madini hayo lipo Mwanadulatu,Mkuranga,Pwani.
MMILIKI wa chimbo la madini ya Ujenzi(Mchanga)lililopo Mwanadulatu,Mkuranga Mkoa wa Pwani,Kitindi Abdallah Langweni(48)(kulia)akiwa na karani wake wakielekea Wizara ya Nishati na Madini,kulipia kodi ya kila mwezi ya chimbo lake.

No comments:

Post a Comment