Clement George Kahama, al-maarufu Sir. George, mmoja kati ya waasisi wa
Taifa la Tanzania Amefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya
Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Clement George Kahama, al-maarufu Sir. George enzi za uhai wake
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kada wa
Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Juma Mwapachu amethibitisha kutokea
kwa kifo cha Sir. George na kusema kuwa amefariki leo saa kumi na dakika
arobaini za jioni.
Sir. George, ni mtumishi wa umma aliyekuwa mtendaji mkuu na mwanasiasa
aliye mahiri na makini, katika utendaji kazi kuanzia nyakati za
Tanganyika kudai uhuru mnamo miaka ya 1950, hadi kujitawala mwaka 1961.
Enzi za uhai wake Sir. George alishawahi kuwa waziri katika wizara
mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti. Mungu ampumzishe mahali pema
peponi.
No comments:
Post a Comment