
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda Jumatatu hii amekabidhiwa na
kuzindua barabara ya kilometa 1 iliyojengwa kwa kiwango cha zege ambayo
inaonganisha kati ya Kurasini na barabara ya Kilwa Road.
Mwaka jana RC Makonda katika harakati za kutatua kero za wananchi
alipewa kero ya barabara hiyo na yeye kuikabidhi kwa kampuni ya
ukandarasi Grant Tech Company ambayo ilijitolea kuikarabati barabara
hiyo kwa kiwango cha zege.
Akiongea katika makabidhiano hayo Operation Manager wa kampuni hiyo, Bw.
Maswingo alisema anayofuraha kumkabidhi mkuu wa mkoa barabara hiyo ya
kimometa 1 ambayo inaonganisha katika ya Kurasini na Kilwa Road ikiwa
imejengwa kwa kiwango cha hali ya juu kutokana na aina ya magari ambayo
yanatumia barabara hiyo.
“Hii barabara aliizindua mkuu wa mkoa mwaka jana mwezi 12 na sasa hivi
tunamkabidhi ikiwa imekamilika. Barabara hii ni kiungo muhimu katika
eneo hili bila shaka itachangia kuchochote maendeleo kwa mkoa wa Dar es
salaam kwa kuwa ni barabara hii ni kiungo muhimu,” alisema Mwaswingo.
Kwa pande wa mkuu wa mkoa Dar es salaam, Paul Makonda alisema barabara
hiyo itakuwa chachu ya maendeleo kwa mkoa wa Dar es salaam kwa kuwa
itawarahishia wafanyabiashara kutoa mizigo yao bandarini kwa urahisi.
“Ni barabara muhimu sana lakini ilikuwa ni barabara mbovu na isiyopitika
hasa katika mazingira ya nyakati za mvua kama hizi. Kwahiyo
niliwatafuta hawa ndugu nikawaomba namna mbavyo wanaweza kutoa mchango
wao katika kuhakikisha hii barabara inapitaka vizuri na walinikubalia
chini ya mkurugenzi wa na kampuni yao kwamba watatoa mchango wa
kuiboresha Dar es salaam mpya kwa namna mbavyo wanaona wao inafaa,”
alisema RC Makonda.
RC Makonda akikagua barabara hiyo
Pia RC Makonda ametoa onyo kali kwa kampuni za ukandarasi zinazofanya
shughuli zao hapa jijini chini ya viwango huku akidai kampuni
zitakazotambuliwa zitatakiwa kurudia miradi hiyo kwa gharama zao binafsi
na kupewa adhabu ya kufungiwa kandarasi yoyote hapa jijini kwa miaka
mitatu.
“Wananchi wamechoka kutengeneza magari kila mara kutokana na ubovu wa
barabara, wakina mama wamekuwa wakijifungulia barabarani hasa nyakati za
mvua kama hizi kutokana na ubovu wa barabara zilizojengwa hata miezi 6
haijapita”.
No comments:
Post a Comment