Hispania .Polisi nchini Hispania wameanza kuchunguza tuhuma zilizotolewa
na maofisa wa klabu ya Real Madrid kwamba kifurushi kilichotumwa kwa
rais wa timu hiyo, Florentino Perez kilikuwa na poda inadhaniwa kuwa ni
sumu.

Tukio hilo lilitokea juzi, hata hivyo uongozi wa timu hiyo umetoa taarifa polisi ili lichunguzwe kwa kina.
Taarifa kutoka vyombo vya habari nchini humo zilieleza kwamba, mzigo huo ulitumwa kutoka Italia.
Wiki hii Real Madrid ilikutana na timu ya Napoli ya Italia kwenye
mchezo wake wa hatua ya 16 bora mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na
Madrid iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kuiondoa Napoli kwa jumla ya
mabao 6-2.
Hadi mapumziko timu hiyo ya Italia ndiyo iliyokuwa ikiongoza kwa 1-0.
Hata hivyo mabao ya Madrid yaliwekwa kimiani na Sergio Ramos aliyepiga
mawili na Alvaro Morata.
No comments:
Post a Comment