Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi
na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (wa kwanza
kulia) akizungumza mapema leo katika kipindi cha JAMBO kinachotangazwa
na TBC One kuhusu Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi
(OPRAS). Wengine katika picha ni Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Mifumo
na Viwango vya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi, Bi. Veila
Shoo (katikati) na Mwongozaji wa kipindi hicho, Bw. Rashid Salim.
Mtangazaji wa Kipindi cha “JAMBO”
kinachotangazwa na TBC One, Bw. Rashid Salim (kushoto) katika mahojiano
na Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya
Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba, pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya
Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi, Bi.
Veila Shoo. Kipindi cha Jambo maudhui yake yalikua kutoa elimu kuhusu
umuhimu wa Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS)
kwa Waajiri na Watumishi wa Umma nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi
na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (kulia)
akifafanua jambo kuhusu umuhimu wa Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini
ya Utendaji Kazi (OPRAS) kwa Waajiri na Watumishi wa Umma mapema leo
katika kipindi cha JAMBO kinachotangazwa na TBC Taifa. Kushoto ni
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kutoka
Ofisi ya Rais – Utumishi, Bi. Veila Shoo. Wengine ni waongozaji wa
kipindi hicho, Bi. Anna Mwasyoke na Bw. Paul Alphonce.
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya
Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi, Bi.
Veila Shoo (kushoto) akizungumza mapema leo katika kipindi cha JAMBO
kinachotangazwa na TBC Taifa kuhusu umuhimu wa Mfumo wa Wazi wa Mapitio
na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) kwa Waajiri na Watumishi wa Umma
nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa
Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba. Wengine ni waongozaji wa
kipindi hicho kushoto ni Bi. Anna Mwasyoke na Bw. Paul Alphonce.
No comments:
Post a Comment