
Mkali wa muziki wa kufokafoka (Hip Hop) nchini, Shariff Thabeet ‘Darassa’, ameendelea kuwa gumzo Afrika ya Mashariki na kila pembe ya ulimwengu kupitia mtandao wake wa YouTube. Mwanamuziki huyo mpaka sasa wimbo wake umetazamwa na watu 3,025,486, idadi ambayo imevunja rekodi kwa wanamuziki wa Bongo Fleva mwenye miondoko ya ‘Hip Hop’.

Waswahili wanasema kizuri kinajiuza, kwani wimbo wa Darassa kwa sasa kila kona unasikika na kuzidi kupokelewa na watu wa kila hisia. Wimbo huo ambao haukuhitaji promo, umekuwa ukiombwa na mashabiki lukuki katika vituo mbalimbali vya televisheni na vya redio.
No comments:
Post a Comment