Sunday, 15 January 2017
Soya: Chakula Chenye Kinga Na Tiba
Mwaka 1999, Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa nchini Marekani (UFDA), iliwaruhusu wasindikaji wa vyakula kutangaza rasmi kuwa soya ni halali na sahihi kutumika duniani kote kama tiba na kinga kwa maradhi ya moyo, yakiwemo shinikizo la damu, kiharusi
Kama vile haitoshi, taasisi nyingi za kupambana na kutibu maradhi ya saratani duniani zimekuwa zikihamasisha matumizi ya lishe ya soya kwa wagonjwa wa saratani za aina mbalimbali baada ya kushuhudia nafuu wanayoipata wagonjwa kwa kutumia bidhaa za soya.
Lakini, wapo ambao ndoa zao zinalegalega kwa kukosa hamu ya ndoa. ‘Saponon’ ambayo imo katika soya ikitumika kwa wiki kadhaa tu hamu hurudi katika hali ya kawaida kwa jinsia zote: wanaume na wanawake ‘Saponon’ huchachua homoni zinazouchangamsha mwili na akili pia.
Ukiachana na faida hizo, zipo nyingine kama vile kutibu mzio (allergy) za aina zote, hukarabati ngozi na hujaza madini ya ‘calcium’ na ‘boron’ kwenye mifupa na kutibu maradhi ya maumivu ya viungo kwa wenye miili mikubwa, wajawazito na wazee pia.
Soya ina madhara yake pia isipotayarishwa ipasavyo. Soya ina chembechembe aina ya ‘purine’ ambazo zimejikita kwenye ngozi yake na zikiliwa, mwili wa binadamu huzigeuza kuwa tindikali iitwayo ‘uric acids’ ambazo ndizo chanzo cha maradhi mengi yakiwemo ya vifundo au ‘gout’, japo ‘uric acids’ hizo hutoka mwilini kupitia mkojo.
Ni vyema ikaeleweka kuwa kula mimea na nafaka ni sawa na kusafirisha madini kutoka ardhini kwenda mwilini. Kitaalamu, unaweza usiipate soya bora kwa kuwa hutoka katika aina tofauti za udongo wenye madini tofauti.
Hapo ningependa kukushauri kuwa kama kweli una nia ya dhati basi tumia soya iliyotoka mikononi mwa wataalam ambao wameiandaa vema soya hiyo ikiwemo kuipitisha katika mamlaka za udhibiti wa vyakula na madawa kama vile TBS na TFDA za hapa nchini ambako huangalia kama hazina sumu zitokanazo na uchafuzi wa mazingira.
Soya inaweza kutumika kama kinywaji chepesi au kama uji au kwa kuchanganywa na unga wa nafaka zingine na kutumika katika kuandaa vyakula vya iana mbalimbali ukiwemo ugali. Hakikisha unapata unga wa soya ulioandaliwa vyema na kuutumia utakavyo ili kuupa mwili wako kinga au kujipa nafuu ya haraka kama ni mgonjwa.
Labels:
MWANZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment