Wednesday, 4 January 2017

Mike Phelan atimuliwa na Hull City

Mike Phelan
Klabu ya ligi kuu ya soka nchini Uigereza, Hull City imemfukuza kocha wake mkuu Mike Phelan, kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo, kwenye ligi.
Phelan, mwenye umri wa miaka 54, alichukua nafasi ya Steve Bruce, kama kocha wa muda na baadaye mwezi Oktoba akapewa mkataba wa kudumu.
Uongozi wa Hull, umesema kwa sasa unamtafuta kocha mwingine, wa kurithi nafasi hiyo.

Hull ipo kwenye nafasi ya kushuka daraja wakifanya vibaya zaidi katika michezo tisa iliyopita, na ndiyo sababu iliyomuondoa Phelan, aliyeshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi Agosti.

No comments:

Post a Comment