Wednesday, 4 January 2017

Maneno aliyosema Farid Musa kuhusu timu yake ya Hispania

Mchezaji wa Tanzania, Farid Malik Mussa amesema kwamba anasubiri leseni ya Mamlaka ya Shirikisho la Soka Hispania (RFEF) aanze kuchezea klabu yake, Club Deportivo Tenerife.
Farid amejiunga na klabu hiyo ya Santa Cruz de Tenerife, Tenerife, visiwa vya Canary mwezi huu kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu kutoka Azam FC ya Dar es Salaam.
Faridi amepost ujumbe kwenye account yake ya Insagram akieleza hali ilivyo baada ya kuwasili kwenye klabu yake mpya ya Tenerife ya Hispania.

“Thanks God nimeanza mazoezi leo na timu yangu mpya wameshanifanyia medical test ninachosubiri sasa ni leseni kutoka chama chao cha mpira cha Spain.”

“Nimeanza maoezi na timu ya U-23 kwa sababu wanajaribu kunifundisha mfumo wanaoutumia kucheza mechi mbalimbali za U-23 huku nikisubiri leseni yangu, kikubwa kwangu namuomba Mungu aendelee kunipa moyo wa subra nina imani kila kitu kitakuwa sawa.”

No comments:

Post a Comment