Masele afunga ndoa
BI Specioza Malick mke wa msanii wa vichekesho nchini aliyejipatia
umaarufu mkubwa kwa mtindo wake wa kuchekesha, Chrispine Lyogello
‘Masele Chapombe’, ni vyema akajitayarisha kucheka na kuvunjika mbavu
kutokana na sanaa hiyo ambayo mumewe anaiweza ilivyo.
Mrembo huyo, aliyefunga ndoa na msanii huyo mwezi huu wa Januari,
ameshauriwa na mashabiki wa sanaa ya mumewe ajitayarishe kucheka zaidi
na wakati huohuo awe na ubavu wa kutenganisha kazi ya Masele na maisha
yake halisi.
“
Mke wa Masele ajiandae kucheka mpaka kuumwa mbavu siku Masele akiamua
kumletea nyumbani vituo anavyofanya kwenye televisheni nyumbani. Bi
Specioza ajiandae kuwa maarufu kwani kwa sasa ameungana mwili mmoja na
mtu maarufu nchini,” alisema shabiki mmoja aliyejitambulisha kama Bondi
Masaba wa jijini Dar es Salaam.
Ndoa ya wawili hao ilifungwa katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira
Maria Consolata lililopo Mbezi-Makabe jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment