Kikao cha kujadili changamoto za
Muungano kinafanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la wawakilishi
Kikwajuni Unguja. Kikao hiki cha ngazi ya Mawaziri kinajumuisha Mawaziri
kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ). Kikao hicho ni utangulizi wa Kikao cha Makamu
wa Rais kitakachofanyika mchana wa leo.
Wa pili kutoka kulia ni Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. January Makamba, akiongea katika kikao cha ngazi ya Mawaziri
kinachohusisha Mawaziri Kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kinachojadili changamoto za Muungano,
Mjini Unguja, wa Pili kutoka Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Pili wa Rais wa (SMZ) Mhe. Mohamed Aboud Mohamed. Kulia kwake ni
Bwana Joseph Abdallah Meza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
(SMZ) na wa kwanza Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamuhuri ya Muugano wa Tanzania Profesa Faustin Kamuzora.
Katika Picha Sehemu wa viongozi wa
Serikali ya (SMZ) katika kikao cha ngazi ya Mawaziri kinachojadili
changamoto cha Muungano Mjini Zanzibar Leo.
(Picha na Evelyn Mkokoi na Lulu Mussa wa OMR)
No comments:
Post a Comment