Hayo yamebainishwa na Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Kalist Lazaro ambapo amesema halmashauri yake imekaa chini na kuona kuliko fedha hizo wapewe wakandasi ili wajenge madarasa ni bora fedha za ujenzi wa madarasa zipelekwe katika kamati za shule pamoja na bodi za shule ili wasimamie ujenzi huo.
Amesema sasa hivi halmashauri imetoa shilingi bilioni moja laki nne kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 56 ya shule za msingi na fedha zote zilishapelekwa katika kamati za shule ili waweze kusimamia ujenzi mpaka ukamilike.
Kalisti amesema zamani walikuwa wanatumia wakandarasi kutangaza tenda kwa ajili ya kujenga madarasa ya shule za msingi lakini tangu waanze kujenga madarasa kupitia kamati za shule na siyo wakandarasi wameokoa milioni 364 ambazo wangetumia wakandarasi zote zingeingia katika mfuko wa mkandarasi
Aidha amesema hadi sasa wameshaandikisha wanafunzi wa darasa la kwaza zaidi ya 12, 000 tofauti na mwaka uliopita 2016 ambapo watoto 9600 waliandikishwa kuingia darasa la kwanza na bado wanaendelea kuandikisha hadi mwezi Machi.
Amesema kutokana na kuwepo na watoto wengi waliojiandikisha kumekuwa na upungufu wa madarasa hivyo halmashauri imejenga madarasa 56 kwa ajili ya watoto hao wapya na kukarabati madarasa manne ya shule ya msingi ambayo yatasaidia kumaliza tatizo Hilo
No comments:
Post a Comment