Monday, 16 January 2017

Israel ipo tayari kufanya mazungumzo ya amani na Palestina"

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov amedokezea kuwa na matumaini kuwa Israel imekuwa tayari kufanya mazungumzo ya amani na Palestina .
"Israel ipo tayari kufanya mazungumzo ya amani na Palestina "
Lavrov alifahamisha kuwa mwaka jana Urusi ilikuwa tayari kuwa mwenyeji wa viongozi wa Palestina na Israel katika mazungumzo hayo na bado Urusi ina nia ya kuhamasisha mazungumzo hayo ili kumaliza mvutano baina ya nchi hizo mbili.
Lavrov alisema haya katika mkutano na katibu mkuu wa shirika la Palestina la ukombozi Saeb Erekat jijini Moscow .
Kwa upande wa mkuu wa mazungumzo kutoka Palestina alifahamisha kuwa wapo tayari kufanya mazungumzo hayo jijini Moscow .

Mazungumzo ya amani katika Mashariki ya Kati yatafanyika jijini Paris Januari 15 na Urusi na itawakilishwa katika mazungumzo hayo na balozi wao nchini Ufaransa .
Hata hivyo waziri mkuu Benjamin Netanyahu wa Israel alisema kongamano la Paris halitafaulu kutatua mzozo baina ya Israel na Palestina .

No comments:

Post a Comment