Bondia Iddi Mkwela akielekezwa kupiga ngumi zenye mkunjo wa chini
‘Upcat’ na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu
Mhamila ‘Super D’ wakati wa mazoezi yanayoendelea katika Super D gym
iliyopo kariakoo shule ya uhuru Mkwela atazipiga na Manyi Issa Feb
5 katika uwanja wa ndani wa Taifa ‘Indoor Stadium’ mpambano wa raundi
kumi uzito wa KG 61
Bondia Iddi Mkwela akielekezwa kupiga ngumi zilizo nyooka na kocha wa
kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ wakati
wa mazoezi yanayoendelea katika Super D gym iliyopo kariakoo shule ya
uhuru Mkwela atazipiga na Manyi Issa Feb 5 katika uwanja wa ndani wa
Taifa ‘Indoor Stadium’ mpambano wa raundi kumi uzito wa KG 61
Na Mwandishi Wetu
Bondia Iddi Mkwela ameingia
kambini baada ya kusaini mpambano wake wa raundi kumi uzito wa kg 61
kupambana na Manyi Issa Feb 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa
Mpambano uho wa mabondia hawo
unatarajia kuwa mzuri sana kwa kuwa mabondia wote ndio kwanza wananza
kuwika katika tasinia ya masumbwi na ndio mpambano uliobeba hisia za
wapenzi na mashabiki wengi wa mchezo wa ngumi kutokana na kutajwa mara
kwa mara kwa wapenzi wa wanaofatilia mchezo wa ngumi kwa sasa nchini
akizungumza kuhusu mpambano wake
uho Mkwela amesema kuwa anae mtafuta sio yeye kabisa kwani ayupo katika
akili yangu kwa kuwa kesha jipendekeza huyu atakuwa kafanywa kafala
kwani ndio njia yangu ya kwenda kwa mabondia ninao wataka huyu sio saidi
yangu ngumi ajajua ili mikono ita ongea siku hiyo sina maneno mengi
alisema Mkwela;
nae kocha wa Kimataifa wa mchezo
wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ anae mnowa bondia huyo
amesema kwa kuwa mpambano wa kwanza kwa Mkwela kucheza raundi kumi
naitaji nimwangalie pumzi yake kwani mazoezi anafanya mengi ya nguvu na
ana bidii ya mazoezi matumaini yangu atashinda ushindi ambao ato
wasumbua majaji kuandika katika karatasi zao yani K.O ya mapema
Ahidha siku hiyo kutakuwa na
mapambano mbalimbali ya kukata na shoka ambapo bondia kutoka mbeya
Meshack Mwankemwa atakumbana na Ramadhani Shauri katika mpambano wa
raundi kumi za ubingwa
Mpambano mwingine utawakutanisha
bondia Mohamed Matumla atakaevaana na Mfaume Mfaume wengine ni Mohamed
Swedi atakae vaana na Ahidar Mchenjo na Ibrahimu Maokola atazipiga na
Zumba Kukwe kutoka Kibaha pamoja na mapambano mengine mbalimbali
No comments:
Post a Comment