Kuna ule msemo maarufu siku hizi, ‘Usiempenda kaja’ ndiyo tunaweza
kusema sasa unatumika kwa watu waliompinga Trump na huku akiwa ameshinda
kiti cha Urais Marekani.

Waliotamka maneno hayo walijiapiza kuwa akishinda watachukua uamuzi mgumu, je, watafanya kama walivyoahidi?
Mwandishi wa Vitabu na mtunga mashairi, wa Nigeria, anayeishi Marekani,
Wole Soyinka, alijiapiza kuwa Trump akishinda atachana kibali maalum cha
kuishi Marekani.
Nyota wa Hollywood Samuel L Jackson alisema atahamia Afrika Kusini iwapo
Donald Trump atashinda uchaguzi wa urais Marekani, tovuti ya News 24
iliripoti.
Mastaa wengine walioahidi kuhama Marekani endapo Trump atashinda ni
pamoja na Miley Cyrus ambaye ni muigizazi. Moja ya muvi alizoigiza ni
Hanna Montana nani Mwanamuziki pia. kupitia ukurasa wake wa Instagram
Cyrus alisema Trump akishinda yeye atahamia Canada.
Muigizaji Neve Campbell na mtunzi wa Filamu Lena Dunham walisema watahamia Canada.
No comments:
Post a Comment