
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Mashaka Gambo akifungua Kikao cha kwanza cha Kamati ya Amani ya viongozi
wa dini Mkoa kilichofanyika Ofisini.

Kamanda wa Takukuru Wilaya ya
Arusha Jacquline Kapila akielezea kazi za Taasisi yake kwa viongozi wa
Dini kwenye kikao cha kamati ya Amani

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo akiongea na viongozi wa Dini wakati wa Kikao cha Kamati ya Amani.

ASKOFU Mkuu wa Dayosisi ya
Kaskazini Kati katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
Mkoani Arusha, Solomon Masangwa akioelezea mchango wa viongozi wa Dini
katika kuhamasisha amani.

Sheikh Mkuu wa Bakwata mkoa wa
Arusha, Shabaan Juma akichangia kwenye Kikao cha Kamati y Amani kwa
kawataka wananchi kudumisha amani na kujenga utamaduni wa kuvumiliana.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA)
Mkoani Arusha Apili Mbaruku akijibu hoja za viongozi wa dini wakati wa
Kikao cha Kamati ya Amani.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Mashaka Gambo(kushoto) katika mazungumzo na ASKOFU Mkuu wa Dayosisi ya
Kaskazini Kati (KKKT) Mkoani Arusha, Solomon Masangwa baada ya Kikao cha
Kamati ya Amani.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Mashaka Gambo(katikati) katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Dini
waliohudhuria Kikao cha Kamati ya Amani.
………………………………………………..
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe
Mrisho Mashaka Gambo amekutana na kamati ya Amani ya Mkoa ambayo
inajumuisha viongozi wa dini mbalimbali zilizoko katoka Mkoa huu
kuzungumzia mustakabali wa Amani na namna viongozi hawa wa dini
watashirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta maendeleo kwa
wananchi ambao ni waumini wao.
Akizungumza katika Kikao hicho
Mhe. Gambo alisema kazi ya Ulinzi wa Amani itakua rahisi sana kupitia
viongozi wa dini ambao wana karama ya kuongea na kubadilisha maisha ya
watu bila kutumia nguvu ama kuwashurutisha isipokua kwa chakula cha
roho ambacho hujenga misingi imara ya imani na tabia njema.
Maendeleo ya wananchi hayawezi
kupatikana bila Amani kuwepo katika Mkoa wetu ni lazima tusaidiane
katika hili dhamira yetu ifanikiwe kwa wepesi zaidi tuna Imani kubwa
sana Na viongozi wetu wa dini na ndio maana nikaona ni vyema tukakutana
ili tusikie kutoka kwenu ninyi ambao mnawakilisha kundi kubwa la
wananchi na pia kufahamu kero mbalimbali zinazowakwaza wananchi katika
maeneo yenu alisema Gambo.
Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini
Kati KKKT Solomon Masangwa akichangia kuhusu masuala yanayoweza
kuhatarisha amani alisema kundi ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa jicho
la Tatu na litasaidia sana katika ulinzi wa Amani ni waendesha boda boda
pamoja na wanachinga ambao kwa sasa wanaonekana kutopewa kipaumbele au
hatuwajali kwa kiasi kinachostahili.
Tunapaswa kuangalia namna gani
watu wanaofanya shughuli hizi wanakua rasmi kwa kupatiwa maeneo maalumu
pamoja na utambulisho utakaowawezesha kufanya kazi zao kwa Amani na
kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao na si kama walivyo sasa
wanafanya kazi hizo katika maeneo yasiyo rasmi na kuhama kila siku hali
hii ina wafanya wajihisi kama si sehemu ya Taifa hili hivyo wanaweza
kutumika kiurahisi kuhatarisha amani ya Nchi yetu alisema Masangwa.
Akichangia katika viashiria vya
uvunjifu wa amani Askofu Dr. Leornard Mwizarubi wa Kanisa la SAYUNI EAG
(T) alisema ni vyema Serikali ikajikita katika kutatua changamoto
zinazoathiri maisha ya kila siku ya wananchi ili hata sisi viongozi wa
dini tunapoongea na waumini tuwe na vielelezo dhabiti vya kuonyesha
namna ambavyo Serikali kero zao zimeshughulikiwa.
Aliendelea kusema “Katika eneo
ambalo ninatoa huduma ya Kiroho kwenye Kata za Unga Ltd, Sokoni 1,
Daraja II, Sinoni na maeneo ya jirani wakazi wa mitaa hiyo wanapata
shida sana ya huduma ya maji Taka na hata katika Kanisa langu
inanilazimu kutafuta gari la kunyonya maji taka mara tatu kwa wiki ili
kufanya mazingira kuwa safi, sasa kuna maeneo mengine wananchi hao
hawana uwezo wa kutafuta gari hilo la kunyonya maji taka hivyo wanaishia
kulalamika kwa kuishi katika mazingira machafu”
Aidha Sheikh Mkuu wa Bakwata mkoa
wa Arusha, Shabaan Juma alishkuru Sekretariet ya Mkoa kwa kikao hiki
muhimu kwa ustawi wa jamii ya Arusha na kueleza kuwa katika kipindi hiki
cha Mpito Nchi yetu inahitaji maombi ya bila kikomo ili kuweza kuvuka
salama na tunategemea kuendelea kuona mabadiliko katika kila eneo;
Tunaamini si wote wanafurahia mabadiliko haya hivyo tuna wajibu wa
kuwajulisha waumini wetu kuhusu umuhimu wa mabadiliko ya mifumo katika
uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano na faida zitakazo patikana kwa
Taifa.
Akiwasilisha changamoto katika
upande wake Sheikh Shaaban alisema “Kuna ukuaji wa kasi ya makazi holela
katika Jiji la Arusha, Utaratibu wa mipango miji hauzingatiwi na hii
inasabisha maeneo mengi kutopitika kwa urahisi hivyo hata itakapotokea
dharua sio tahisi kwa wananchi wetu kupata msaada wa haraka, tunaomba
wanachi wapimiwe maeneo yao, barabara zifunguliwe ili huduma muhimu
ziweze kufika katika maeneo hayo”.
Mkurugenzi wa Idara ya maji safi
na maji Taka (AUWASA) Eng. Ruth Koya alisema Taasisi yake inaanza
utekelezaji wa Mradi mkubwa wa maji safi na Taka ambao matatizo yote
yaliyowasilishwa katika kikao hiki yanayohusiana na maji yatashughuliwa
kupitia mradi huo.
Aliongeza kuwa mradi huo
utahusisha uboreshaji wa mioundombinu ya maji safi, Uhamishaji wa
mabwawa ya maji Taka(yaliyokuwa Lemara kwa hivi sasa), ununuzi wa magari
ya kunyonyea maji machafu pamoja na magari ya kusambaza na kuuza maji
safi.
Mkuu wa Mkoa Mge. Gambo alitolea
ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa na kuelezea namna ambavyo
Changamoto ya Mipango Miji ilivyopata ufumbuzi kupitia ukamilishaji wa
Mpango Mkakati wa Jiji la Arusha (Master Plan) na kuwajulisha wajumbe
kuwa mpango umekamilisha na umekwishapitiwa na Halmashauri zote tatu
zinazohusika, hivyo kwa hivi sasa utawasilishwa Wizarani na taratibu
zote zikikamilika utekelezaji utaanza mara moja.
Kuhusu suala la Machinga na
waendesha boda boda boda Rc Gambo alisema Serikali imekwisha anza
utaratibu wa kutafuta maeneo salama na rafiki kwa ajili ya
wafanyabishara ndogondogo maarufu kama machinga na tutaongea nao ili
tuwe na makubalino ya pamoja.
Aidha kuhusu bodabdoa tumeanza
kuwatambua kupitia kwenye uongozi wa mitaa na vituo vyao na
tutahakikisha tunaboresha mazingira yoa ya kufanyia kazi na zaidi
tunawatafutia Pikipiki ambazo watapewa Vijana wanaofanya biashara ya
boda boda kwa utaratibu maalumu; Itawapasa kurudisha Fedha za Pikipiki
tu na kisha kupata umiliki halali ya Chombo hicho tofauti na sasa hivi
ambapo wanapewa pikipiki hizo na kulipa mara mbili ya bei kwa matajiri
wao ndipo wapate Umiliki alimalizia Gambo.
No comments:
Post a Comment