Friday, 18 November 2016

Vyeti vya kuzaliwa watoto kutolewa ofisi za kata

Dar es salaam. Wakala wa usajili, ufilisi na udhamini (Rita)  imesema vyeti vya kuzaliwa kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 5 sasa vinatolewa bure katika vituo vya huduma ya uzazi na ofisi za mtendaji wa kata.
Kaimu Mkurugenzi wa Rita, Emmy Hudson amesema mpango huo ulibuniwa mahususi kwa ajili ya kutatua changamoto ya watoto kushindwa kupata vyeti vya kuzaliwa kutokana na bei ua mlolongo wa upatikanaji wake.



"Tayari tumetoa elimu kwa watakaohusika na utoaji wa vyeti hivyo na taasisi kama majeshi, uhamiaji na shule ambao huhitaji vyeti hivyo kwaajili ya kujiridhisha na taarifa za watu sasa  watavitambua vyetu hivyo kuvitambua vyeti hivyo kama vyeti halali vilivyotolewa na mamlaka ya Serikali," alisema Hudson.

No comments:

Post a Comment