Zoezi la kusaka vipaji katika klabu ya Azam
Klabu ya Azam FC, inatarajia kuendelea na mpango wake wa kitaifa
wa kusaka wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 (U-17) Jumamosi
Novemba 19, mwaka huu (kesho) katika Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya
kuanzia saa 1.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana
Azam FC wikiendi iliyopita iliendesha zoezi hilo Dar es Salaam
lililohudhuriwa na vijana 433 na kuchaguliwa saba pekee, na hivyo
kufanya idadi kamili ya waliochaguliwa kwenye mchujo wa kwanza kufikia
50 miongoni mwa vijana 2,593 walisailiwa mpaka sasa katika maeneo manne
ambayo Azam FC imeendesha zoezi hilo (Dar es Salaam, Tanga, Morogoro
& Dodoma na Visiwani Zanzibar).Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imeeleza kuwa mara baada ya zoezi hilo kukamilika kwenye maeneo yote, vijana wote watafanyiwa mchujo wa mwisho mwezi ujao katika Uwanja wa Azam Complex kabla ya timu hiyo kuundwa rasmi kwa vijana bora watakaofanya vizuri kuchukuliwa.
Imesema vijana wanaotakiwa kuhudhiria zoezi hilo na wale walizaliwa kuanzia mwaka 2000, 2001, 2002, 2003 au 2004, ambapo uhakiki wa vyeti utafanyika kwa wale watakaochaguliwa.
Klabu hiyo pia imesema kuwa majaribio mengine ya wazi katika maeneo mengine kuzunguka Tanzania yatatangazwa hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment