Serikali ya Urusi imetangaza kuidhinisha uamuzi wa kutaka kujitenga na mahakama kuu ya kimataifa.
Kulingana na maelezo yaliyotolewa na ikulu ya Kremlin, iliarifiwa kwamba
rais Vladimir Putin ametia saini rasimu ya uamuzi huo wa kutaka
kujitenga na mahakama kuu ya kimataifa kufuatia pendekezo la wizara ya
sheria na masuala ya nje.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba Putin pia alitoa agizo la kuwasilishwa
kwa uamuzi huo kwa ofisi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitriy Peskov alifahamisha kuchukuliwa kwa
uamuzi huo kutokana na vizuizi vya sheria vilivyopo kwa taifa la Urusi.
Wizara ya masuala ya nje ya Urusi pia ilikahsifu mahakama kuu ya
kimataifa kwa ukosefu wa haki na uadilifu katika sheria kutokana na
kushindwa kujitegemea.
Mahakama hiyo pia inadaiwa kuangazia mzozo wa Georgia wa mwaka 2008 kwa upande mmoja na kughadhabisha Urusi.
No comments:
Post a Comment