Mapacha Charlotte na Olivya
Mwanamke raia wa Australia aliyeambiwa na madaktari kuwa hawezi kutunga
mimba amejifungua mapacha wanaodaiwa kutungwa siku tofauti. Kate Hill
alikua akipokea matibabu ya kumuwezesha kutunga mimba.Wakati wa matibabu hayo alitunga mimba za mapacha walioachana kwa siku kumi. Hatua kama hii huwa ni nadra sana na watafiti wanaiita 'Superfestation', ambapo mwanamke huweza kutunga mimba nyingine wakati tayari akiwa mja mzito.
Kate Hill na Mumewe Peter Hill wazazi wa mapacha hao
Mapacha hao wasichana, Charlotte na Olivia wana miezi kumi sasa lakini
walizaliwa na uzito tofauti na hata maumbile.Kate Hill amesema
waligundua maajabu ya wanao baada ya kuzaliwa.Katika hali hiyo inayojulikana kama 'superfestation', mwanamke huendelea kupata hedhi hata haada ya kutunga mimba na ndio maana bi Hill alitunga mimba baada ya siku kumi za uja uzito wa kwanza.
Ni visa kumi tu vimenakiliwa duniani vya watoto waliozaliwa kwa mazingira sawa na mapacha hawa.
No comments:
Post a Comment