Carlos Tevez atakuwa anafikisha miaka 33 mwezi February 2017, lakini ofa
kutoka katika ligi kuu ya China maarufu kama Chinese Super League
inaweza kumfanya akasherekea siku yake ya kuzaliwa kama mchezaji
anayelipwa zaidi duniani.
Vilabu vya China vimeibuka ghafla na kulipa fedha nyingi siku za
karibuni na majina kama Alex Teixeira, Jackson Martinez na Ramires na
wengine wengi huku jina la Tevez likisemekana kuwa linalofuata na
anakadiriwa kuwa atalipwa Euro milioni 40 kwa msimu, ambayo ni zaidi ya
bilioni 90 za kitanzania.
Tarrifa iliyovujishwa na Yahoo Sports Brazil, inasema kuwa klabu moja
kutoka china pia ipo tayari kumlipa Tevez (El Apache) asilimia 60 (60%)
zaidi ya kile anachopokea Lionel Messi na Neymar pale Barcelona ambayo
inakaridirwa kuwa Euro millioni 25.
Ikumbukwe kuwa Februari mwaka huu, Carlos Tevez alipiga chini ofa ya
kujiunga na klabu ya Shanghai SIPG ambayo iliweka mezani kiasi cha Euro
milioni 22 kwa mwaka na aliamua kubaki na klabu ya Boca Juniors.Hii ofa
mpya inatizamiwa kumfanya atamani kwenda katika bara la Asia hilo.
Graziano Pelle kwa sasa anapokea kiasi cha Euro milioni 16m kwa msimu na
klabu ya Shandong Luneng, huku Ezequiel Lavezzi, Ramires na Asamoah
Gyan wote wakiwa wanapokea Euro milioni 13
No comments:
Post a Comment