Rapper
SIMBA SC inatarajiwa kurejea leo jioni mjini Dar es Salaam kwa ndege na
moja kwa moja kuingia kambini, Ndege Beach kujiandaa na mchezo ujao wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba itawasili jioni ya leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA), ikitokea Mwanza ambako itapita kuunganisha usafiri wa
anga baada kusafiri kwa barabara kutoka Shinyanga.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara
ameiambia Fofam-mediablog kwamba mara kikosi kitakapowasili
kitakwenda moja kwa moja kambini Ndege Beach, Mbweni, nje kidogo ya Dar
es Salaam.
Simba SC inarejea leo jioni mjini Dar es Salaam kwa ndege na moja kwa
moja kuingia kambini, Ndege Beach kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara
Manara alisema kikosi kitafanya mazoezi ya siku moja kesho kabla ya
kuingia kwenye mchezo wake mwingine wa Ligi Kuu dhidi ya African Lyon
Jumapili Dar es Salaam.
Ikumbukwe jana Simba imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya timu ngumu msimu
huu, Stand United ya Shinyanga.
Ushindi huo, unaifanya Simba SC ifikishe pointi 35 baada ya kucheza
mechi 13, wakati Stand inabaki na pointi zake 22 za mechi 14.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa, Shomary Lawi wa Kigoma
aliyesaidiwa na Mirambo Tshikungu na Robert Ruhemeja, Simba walipata bao
lao mapema kipindi cha kwanza.
Bao hilo lilifungwa na winga machachari wa Wekundu hao wa Msimbazi,
Shizza Ramadhani Kichuya kwa penalti dakika ya 33 baada ya mshambuliaji
Mrundi, Laudit Mavugo kuangushwa na beki Adeyum Ahmed kwenye boksi.
Baaada ya bao hilo, timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu, lakini ni Simba SC waliokuwa waking’ara uwanjani.
Mapema dakika ya nane, Kichuya aliunganishia nje kwa kichwa krosi ya
beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kabla ya Nahodha wa Stand United,
Jacob Massawe kupiga juu kufuatia krosi ya Frank Hamisi.
Kipindi cha pili, mchezo uliendelea kuwa wa mashambulizi ya pande zote
mbili, lakini Simba inayofundishwa na Mcameroon, Joseph Marius Omog
ilifanikiwa kuulinda ushindi wake.
Na Simba SC ilikaribia kupata bao la pili dakika ya 65 kama si kiungo
Mohamed ‘Mo’ Ibrahim kupiga juu ya lango kufuatia pasi nzuri ya Kichuya.
No comments:
Post a Comment