Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habara, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Geita, Constantine Kanyasu (CCM).
Mbunge huyo alitaka kujua iwapo serikali haioni kwamba uamuzi yaliyofanywa kinadharia na uonevu mkubwa kwa timu hiyo huku akiutuhumu uongozi wa TFF.
Nape amesema katika uamuzi uliochukuliwa na TFF ulikuwa sahihi na ulikuwashirikisha watu wengi.
Hata hivyo, amesema kuna vyombo mbalimbali ikiwemo Takukuru vinaendelea kuwachunguza baadhi ya watendaji ikiwemo ndani ya TFF na kuwa wakati wowote watatoa majibu ya nini kifanyike.
Ameutaka uongozi wa timu ya Geita kuchukua uamuzi ikiwemo kutafuta haki yao mbele zaidi ya TFF kwa kuwa chombo hicho siyo cha mwisho katika kuwapatia wanachotaka.
No comments:
Post a Comment