Na Mwandishi wetu, Dodoma
Kambi Rasmi ya upinzani Bungeni
yaikubali Bodi ya Ithibati, Baraza Huru la Habari pamoja na Bima ya Afya
kwa waandishi wa habari nchini.
Akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi
ya Upinzani Bungeni mjini Dodoma, Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo katika
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Joseph Mbilinyi amesema
kuwa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 unamaufaa kwa
wanahabari nchini
“Kifungu cha 58 kinatoa jukumu na
kuwataka waajiri wa waandishi wa habarikuhakikisha kuwa waandishi wa
habari wanakuwa na bima ya afya pamoja na kuhakikisha kuwa wanachangia
katika mifuko ya hifadhi za jamii” alisema Mbilimnyi.
Msemaji huyo aliendelea kusema “Jambo hili ni jema sana na Kambi Rasmi ya Upinzani inaliunga mkono”.
Kuanzishwa kwa Bodi ya Ithibati
pamoja na Baraza Huru la Habari ni jambo jema vitu ambavyo vitalinda
maslahi ya mwandishi wa habari kwa kuzingatia kuwa moja ya kazi Baraza
na Bodi ni kuweka viwango vya uangalizi pamoja na utaratibu wa kitaaluma
katika kuratibu tasnia ya habari nchini.
Mbilinyi ametoa rai kwa Wabunge
wote bila kujali itikadi za vyama kutambua kuwa jukumu la kutunga sheria
ni wajibu wao wa kikatiba ambayo wanawajibika wakiwa sehemu ya Bunge
kufanya kazi kwa maslahi mapana ya taifa.
Aidha, Mbilinyi amesisitiza kuwa
katika Mkutano wa Nne wa Bunge la 11 Septemba 15 mwaka huu, Serikali
ilileta Muswada wa Huduma za Habari na kusomwa mara ya kwanza kwa lengo
la kuwapa nafasi Wabunge pamoja na wadau mbalimbali wa habari kupitia na
kuufanyia tafakuri ya kina na hatimaye kutoa ushauri kwa Serikali
kuhusu Muswada huo.
Naye Wiziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema kuwa mageuzi katika tasnia ya
habari nchini yataifanya kuwa taaluma kamili itakayowaletea heshima
wanahabari na taifa kwa ujumla.
Kupitishwa kwa Muswada wa Sheria
ya Huduma za Habari itatoa wigo mpana kwa wanahabari kutekeleza majukumu
yao kw uhuru ya kukusanya, kuhariri na kuchapisha au kutangaza habari.
Waziri Nape ameongeza kuwa pamoja
na maboresho mengi ya Muswada huo pia unzingatia suala la mitambo ya
kuchapisha magazeti na majarida nalo limepewa uzito unaostahili kwa
kutohusika moja kwa moja kwa kosa la gazeti ambalo limechapisha habari
yenye makosa ya kisheria dhidi ya watu au taasisi mbalimbali.
Akinukuu maneno mbalimbali ya watu
maarufu duniani juu ya masuala ya habari akiwemo Rais wa Marekani
Thomas Jefferson Januari 16, 1789, Rais wa zamani wa Afrika Kusini
Nelson Mandela, Muasisi wa Taifa la India Mahatma Ghandhi, Baba wa Uhuru
wa Habari John Stuart Mill (1806-1873) pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere, Waziri Nape alimesma kuwa mmoja wa viongozi hao Mahatma
Ghandhi aliamini kuwa uhuru wa kweli wa kujieleza ni ule unaoweka mbele
heshima ya watu wengine na kuwalinda dhidi ya dhara, kebehi, kejeli na
madhara mengine huku Baba wa Uhuru wa Habari John Stuart Mill
akibainisha dhima ya uhuru wa vyombo vya habari na umuhimu wa kuwa huriu
unapaswa kuzingatia ukomo wa haki ya kupata habari kuwa unakoma pale
haki za watu wengine zinapoanzia.
Akichangia katika mjadala wa
Muswada huo wakati, Mbunge Sixtus Mapunda amesema kuwa kwa muda mrefu
tasnia ya habari haikuwahi kupata hadhi inayostahili ndani ya nchi
pamoja na kazi nzuri ya kuhabarisha, kufundisha, kukosoa na kuwasaidia
watu watu wenye matatizo wenye changamoto mbalimbali hata kufikia hadhi
ya kuitwa muhimili wan ne wa dola.
“Tasnia hii haikuwahi kulindwa,
tasnia hii haikuwahi kuenziwa, tasnia hii haikuwahi kuheshimiwa
inayostahili, kwa mwandishi wa habari mwenyewe, kwa chombo cha habari na
wamiliki wa chombo cha habari tofauti na tasnia nyingine nyingine, kwa
mara ya kwanza ndani ya nchi hii, heshima ya tasnia inapatikana” alisema
Mapunda.
Mapunda ameitaja tasni hizo kuwa
ni za Madaktari, Wahasibu na Wahandisi ambao wanachombo chao
kinacholinda maslahi yao, maadili yao na kinachowalinda ili kuendelea
kulinda taaluma yao.
Aidha, Mapunda amesema kuwa kwa
miaka miaka zaidi ya 23, Muswada utasaidia kutatua matatizo yote
yaliyokuwa yanatokana na mapungufu ya Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976
kwa kuwa na Bodi ya Ithibati, Baraza Huru la Habari, Bodi ya Ithibati
Mfuko wa Mafunzo ambayo ni mambo mapya.
Zaidi ya hayo, Mapunda aliongeza
kuwa watu wenye vipaji vya kuandika habari kulingana na taaluma zao
ikiwemo uchumi hawajazuiliwa na Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa
mwaka 2016.
Chimbuko la Muswada huo linatokana
na baadhi ya vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
baada ya kufanyiwa marekebisho mwaka 1984 ambapo haki ya kikatiba ya
kutafuta, kupokea na kutoa habari imeainishwa kwenye Ibara ya 18 (b)
pamoja na mikataba mbalimbali ya kimataifa ya inayoainisha haki na
wajibu wa sekta ya habari.
Mkataba huo wa Kimataifa ni ule wa
Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966 ambao Tanzania iliuridhia Juni
11, 1984 pamoja na Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu 1981
ambao nao uliridhiwa Februari 18, 1984.
No comments:
Post a Comment