Thursday, 10 November 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Magufuli leo ameongoza viongozi na umma wa watanzania katika shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mungai

  mung3
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye wakati wa shughuli za kuagwa kwa mwili wa aliyekuwa kuwa Waziri wa zamani wa Serikali, Joseph Mungai aliyeagwa leo katika ukumbi wa karimjee Jijini Dar es Salaam.
mung4
Rais Dkt. John Pombe (wa tatu kulia) akiwa katika ibada maalum ya kumwombea aliyewahi kuwa Waziri wa zamani wa Serikali, Joseph Mungai aliyeagwa leo katika ukumbi wa karimjee Jijini Dar es Salaam.
mung5
Familia ya Hayati, Joseph Mungai wakifuatilia kwa makini shughuli za kuagwa kwa mwili wa Waziri huyo wa zamani wa Serikali zilizofanyika leo katika ukumbi wa karimjee Jijini Dar es Salaam.
mung6
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitoa salamu za mwisho kwa mwili wa aliyewahi kuwa Waziri wa zamani wa Serikali, Joseph Mungai aliyeagwa leo katika ukumbi wa karimjee Jijini Dar es Salaam.
mung7
Makamu wa Rais mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa salamu za mwisho kwa mwili wa aliyewahi kuwa Waziri wa zamani wa Serikali, Joseph Mungai aliyeagwa leo katika ukumbi wa karimjee Jijini Dar es Salaam.
mung8
Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba akitoa salamu za mwisho kwa mwili wa aliyewahi kuwa Waziri wa zamani wa Serikali, Joseph Mungai aliyeagwa leo katika ukumbi wa karimjee Jijini Dar es Salaam.
mung9
Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye akitoa salamu za mwisho kwa mwili wa aliyewahi kuwa Waziri wa zamani wa Serikali, Joseph Mungai aliyeagwa leo katika ukumbi wa karimjee Jijini Dar es Salaam.
mung10
Waombolezaji wakipita katika jeneza la aliyewahi kuwa Waziri wa zamani wa Serikali, Joseph Mungai wakati wa shughuli za kuagwa kwa mwili wa Kiongozi huyo leo Jijini Dar es Salaam.
mung1
Rais mstaafu, Benjamin Mkapa akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva wakati wa shughuli za kuagwa kwa mwili wa aliyekuwa kuwa Waziri wa zamani wa Serikali, Joseph Mungai aliyeagwa leo katika ukumbi wa karimjee Jijini Dar es Salaam.
mung2
Baadhi ya Viongozi waandamizi kutoka  Chama cha Mapinduzi (CCM) na UKAWA wakifuatilia shughuli za kuagwa kwa mwili wa aliyekuwa Waziri wa zamani wa Serikali, Joseph Mungai aliyeagwa leo katika ukumbi wa karimjee Jijini Dar es Salaam.

NA IMMACULATE MAKILIKA- MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mheshimiwa John Magufuli leo ameongoza viongozi mbalimbali pamoja na  umma wa watanzania  katika shughuli ya kuaga mwili wa marehemu John Mungai katika viwanja vya Karim jee vilivyopo jijini Dar es salaam.
 
Akizungumza kwa niaba ya Serikali  wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano  wa Afrika Mashariki  Balozi Augustine Mahiga alisema kuwa  marehemu Joseph Mungai alikuwa na kipaji cha pekee cha uongozi kwa vile alipewa madaraka makubwa katika umri mdogo na katika wakati mgumu katika historia ya nchi.
“Baada tu ya Azimio la Arusha mwaka 1967 aliyekuwa  Rais wa  Awamu ya kwanza Mwl. Julius  Nyerere  alimteua marehemu Mungai  kuwa Waziri wa Kilimo wakati ambao kulikua na falsafa za  siasa ni kilimo na  kilimo ni uti wa mgongo, hakika Mwl. Nyerere alimuona ni kiongozi aliyefaa” alisema Balozi Mahiga
Ameongeza marehemu amejionesha katika ustawi wa jamii kwa kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii pamoja na kusaidia kaya masikini.
Kwa upande wake, mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru alisema kuwa marehemu Mungai alikuwa kiongozi mahiri na mzalendo, ambaye alijenga shule  za sekondari zaidi ya saba huko mkoani Iringa ambapo baadae alizikabidhi Serikalini kwa maendeleo ya Taifa.
Naye msemaji wa Serikali ambaye ni mtoto wa marehemu Bw. Jimmy Mungai kwa niaba ya familia ameishukuru  Serikali, viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kwa kuendelea kuwafariji katika kipindi hiki kigumu.
Marehemu Joseph Mungai amefariki Dunia ghafla Novemba 8, mwaka huu na    aliwahi kushika nyazifa mbalimbali  serikalini  ikiwemo uwaziri kwa awamu nne za serikali, pia alichaguliwa   kuwa mbunge akiwa na miaka 26 na kuwa mbunge mwenye umri mdogo kuliko wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Viongozi mbalimbali akiwemo Rais Mstaafu  wa Awamu ya Tatu mheshimiwa Benjamini Mkapa,  Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, Makamu Mwenyeliti wa Chama cha Mapinduzi Bara Mheshimiwa Philip Mangula na  Spika wa Bunge Mstaafu  Mheshimiwa Pius Msekwa walijumuika kuaga mwili wa marehemu Joseph Mungai utakaosafirishwa kesho kuelekea mkoani Iringa na  kuzikwa jumamosi saa nane mchana.

No comments:

Post a Comment