Maafisa wamesema kuwa watasambaza rasimu ya azimio kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati kukiwa na wasiwasi wa uwezekano wa kuzuka mauaji ya halaiki kama mgogoro unaoendelea wa kikabila hautasitishwa.
Mapigano yameendelea licha ya kuwapo muafaka tete wa amani kati ya rais wa nchi hiyo Salva Kiir na makamu wake wa zamani Riek Machar kusitisha vita vya karibuni vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Uchanguzi mkuu Sudani kusini ulistahili kufanyika mwezi huu ambapo wapiga kura nchini DRC walistahii kupiga kura mwezi huu kumchagua mrithi wa Rais Kabila, wakati wa kumalizika kwa muhula wake wa mwisho.
No comments:
Post a Comment