Na.Alex Mathias.
Pazia
la Ligi Kuu nchini Kenya mzunguko wa 15 unatarajia kufungwa Leo majira
ya saa kumi na moja jioni kwa upande wa Afrika Mashariki timu nane
kushuka uwanjani huku bingwa tayari ameshajulikana ni Tusker FC .
Mchezo
ambao unaonekana kuwa na watazamaji wengi ni mchezo wa Gor Mahia ambao
msimu uliopita walikuwa mabingwa watakuwa nyumbani kucheza na bingwa
anayeenda kutawazwa timu ya Tusker ambao wataiwakilisha Kenya katika
michuano ya klabu bingwa Afrika CAF.
Gor
Mahia wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 54 na wanahitaji
kushinda ili kuwatimulia raha mashabaki wa Tusker ambao wanaenda
kutangazwa kuwa bingwa wakati Tusker wao wana pointi 58 hivyo wanaingia
uwanja kwa ajili ya kulinda heshima ya kukataa kufungwa na watataka
kushinda ili wachukue ubingwa wao kwa ufalme huku wakiwa wamemfunga
aliyekuwa bingwa msimu uliopita.
Ligi
Kuu ya Kenya inajumuisha jumla ya timu 16 ambazo hushiriki huku mbili
huwa zinashuka daraja na tayari Sofapaka na Nairobi City wameshashuka
msimu ujao hawataonekana tena na watacheza Ligi daraja la kwanza ambalo
ni kungumu kurudi Ligi Kuu kutokana na ushindani uliopo huku chini.
Vita
nyingine ipo katika kuwania kiatu cha dhahabu cha ufungaji magoli msimu
huu kwani kuna watu wawili wanakimbiza kati ya John Makwatta
anayechezea Ulinzi Stars akiwa na magoli 16 na mwingine anayeonekana
kuwania ni Kelvin Aswani anayecheza Leopards akiwa na magoli 14 hivyo
anatakiwa afunge magoli matatu na kumuombea mabaya Makwatta asifunge ila
bahati ya ufungaji inaonekana kuwa itachukuliwa na mshambuliaji wa
Ulinzi Stars.
No comments:
Post a Comment