
Kwa sasa kilicho kwenye akili za wengi ni kuhusu nani watapewa nyadhifa
za juu kwenye uongozi wa rais aliyechaguliwa nchini Marekani Donald
Trump.
Wakati wa hotuba yake ya ushindi, Trump aliwasifu wale waliosimama naye
ambao mara nyinyi wanaonekana kuwa wanaosubiri kujiunga kwenye baraza
lake la mawaziri
Wasaidizi wake walikuwa tayari walikuwa wamesambaza majina ya watu ambao
walionekana kuwa bora kwa baraza la mawaziri siku za mwisho mwisho za
kinyanganyiro cha kuwania urais
Hawa ni baadhi ya wale ambao wanaonekana kuwa huenda wakajiunga na baraza hilo.

Newt Gingrich - Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni
Alikuwa mfuasi wa Trump ambaye aliingia kwenye orodha ya wale
waliotarajiwa kuwa wagombea wenza wa Trump, na ametajwa kuwa
mwanadiplomasia wa hadhi ya juu nchini Marekani
Alikuwa spika wa bunge la wawakilishi mwaka 1994.
Gingrich mwenye umri wa amiak 73 alishindwa wakati alijaribu kuwania uteusi wa kuwa mgombea urais wa Republican mwaka 2011.
![]() |
Newt Gingrich |
Rudy Giuliani - Mwanasheria mkuu
Ni mmoja wa wafuasi sugu wa bwana Trump. Anatajwa kuwa mtu anayeweza kupewa wadhifa wa mwanasheria mkuu nchini Marekani.
Akiwa meya wa mji wa New York wakati wa shambulizi la Septemba mwaka 2011, alipata umaarufu mkubwa wakati huo.
Giuliani ashahudumu kama mkuu wa mashtaka wa jimbo la New York. Pia
aliwania uteuzi wa urais wa chama cha Republican mwaka 2008, lakini
akajiondoa baada ya kushindwa na John McCain na Mitt Romney wakati wa
mchujo.
![]() |
Rudy Giuliani |
Reince Priebus - Mkuu wa watumishi wa Rais
Bwana Priebus mwenye umri wa miaka 44 anaonekana kuwa mtu anayeweza kupewa wadhifa wa kusimamia masuala ya ikulu
Ni rafiki wa karibu wa spika Paul Ryan, ambaye anaonekana kuwa muhimu katika kutekeleza masuala ya ungozi wa serikali mya.
![]() |
Reince Priebus |
Chris Christie - Waziri wa biashara
Baada ya kuzindua kampeni yake ya kuwania urais mwaka huu, gavana huyo wa New Jersey alimuunga mkono bwana Trump
Bwana Christie mwenye umri miaka 54 ametajwa kwa nyadhifa tofauti ikiwemo ya waziri wa biashara.
Lakini amekumbwa na kashfa inayohusu kufunga kwa daraja linalounganisha
majimbo la New Jersey na New York kwa madai ya kumuadhibu meya wa eneo
hilo.
![]() |
Chris Christie |
Jeff Sessions - Waziri wa ulinzi
Ni seneta kutoka Alabama ambaye anatajwa kuwa anayeweza kuwa mkuu wa ulinzi.
Trump alimsifu Sessions wakati wa sherehe ya ushindi mjini New York.
![]() |
Jeff Sessions |
Sessions mwenye umri wa miaka 69 aliunga mkono uvamizi nchini Iraq mwaka 2003.
Michael Flynn - Mshauri wa masuala ya ulinzi
Bwana Flynn ni mwanajeshi mstaafu ambaye alimsaida Trump, kuwafikia wanajeshi wastaafu licha ya Trump kutohudumu katika jeshi.
Anasema alilazimishwa kuacha wadhifa wake kama mkurugenzi wa ujasusi
kati ya mwaka 2012 na 2014 kutokana na maoni yake kuhusu siasa kali za
kiislamu.
![]() |
Wakati wa kampeni alikosoa sera za utawala wa Rais Obama dhidi ya kundi la Islamic State.
Steven Mnuchin - Waziri wa fedha
Trump mwenyewe amemtaja mwenyekiti wa masuala yake ya fedha kwa wadhifa wa waziri wa fedha.
Mr Mnuchin alipata utajiri wake katika kipindi cha miaka 17 alihudu
katika kampuni ya Goldman, kabla ya kuanzisha kampuni yake ya filamu.
![]() |
Steven Mnuchin |
No comments:
Post a Comment