Thursday, 10 November 2016

Bunge labaini ufisadi ujenzi wa machinjio Dar

Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania limebaini ubadhirifu wa zaidi ya shilingi bilioni 4.3 katika uwekezaji wa mradi wa kujenga machinjio ya kisasa Jijini Dar es Slaam, huku meneja wa mradi huo akiwa ameshalipwa zaidi ya shilingi milioni 783.Tokeo la picha la BUNGE LA TANZANIA
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali za Mitaaa (LAAC), Vedasto Ngombare Mwiru, katika taarifa yake kuhusu hesabu zilizokaguliwa na kamati ya hesabu za Serikali za Mitaa kwa mwaka 2013/2014 na 2014/2015.
Katika mradi huo uliokuwa ujengwe eneo la Gongo la Mboto Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam, iliwekeza kupitia kampuni ya nyama iliyoianzisha ya East Africa Meat Company Ltd, lakini mradi huo haukuweza kufanyika kwa kiasi cha pesa kilichopangwa.
Aidha kati taarifa hiyo imeonesha maeneo 10 nyenye matatizo sugu ya matumizi ya fedha za serikali za Mitaa, ikiwemo eneo la manunuzi yasiyozingatia sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment