Lori moja la mafuta limelipuka kaskazini mwa Msumbuji na kuua watu 73 na kuwajeruhi wengine zaidi ya mia moja.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, mlipuko huo ulitokea baada ya wakaazi kukusanyika karibu na lori hilo kwa lengo kununua mafuta ambapo miili kadhaa ambayo imeungua kabisa imeonekana kutapakaa karibu na eneo kulikotokea mlipuko huo.
Maafisa wa serikali wanaamini kuwa miili zaidi huenda iko katika vichaka vilivyo karibu kufuatia habari kwamba baadhi ya watu waliokuwa wameungua vibaya walikuwa wakijaribu kujirusha ndani ya mto ulio
karibu ili kupunguza maimivu makali ya moto.
Chanzo cha mlipuko huo hakikubainika mara moja lakini ingawa kulikuwa na habari kwamba viongozi wa serikali ya Msumbiji walitarajiwa kuwasili katika eneo kujionea hali halisi na kuangalia zoezi la kuokoaji linavyoendelea.
No comments:
Post a Comment