Katika
Kipindi cha miezi nane kuanzia Julai 2015 hadi Februari mwaka huu,
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imekusanya jumla ya Sh Trilioni
8,569,854.40 ikilinganishwa na lengo la kukusanya Sh trilioni 8,685,991.52 ambayo ni sawa na asilimia 99 ya makusanyo yote.
Hayo
yamesemwa leo na Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Alphayo Kidata
wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa Ukusanyaji
wa mapato, matumizi ya mashine za EFDs, kusitisha kwa bei elekezi Na
usajili wa vyombo vya moto.
Amesema
lengo la Mamkala hiyo ni kukusanya Trilioni 12.3 hadi ifikapo Juni Mwaka huu na kwamba asilimia moja iliyobakia katika kukamilisha asilimia
100 ya Ukusanyaji wa mapato kati ya Julai mwaka jana hadi Juni mwaka
huu, itakamilika ndani ya miezi nne iliyosalia ambayo itaisha Juni
mwaka huu.
Amesema pia kwa mwezi Februai pekee. Mamlaka hiyo imefanikiwa kukusanya Mapato ya kiasi cha shilingi trilioni 1,040,540.20 kwa
upande wa Tanzania Bara na Zanziba ambayo kiasi hicho ni sawa na
asilimia 101.18 ya lengo la ukusanyaji ambayo ilikuwa ni Sh Trilioni
1,028,379.40 kwa mwezi.
Amesema
kuongezeka kwa mapato haya kunatokana na kudhibiti kwa mianya ya
ukwepaji wa kodi na kuweka mazingira rafiki kwa mlipa kodi, kurekebishwa
kwa Misamaha ya kodi ambayo ilikuwa inachangia upotevu wa mapato,
kuongezeka kwa watumiaji wa mashine za EFDs pamoja kudhibiti eneo la
forodha ambalo lilikuwa linasababisha upotevu wa mapato ya TRA.
Maeneo yaliyochangia kuongezeka kwa mapato hayo:
“Maeneo
ambayo yamechangia kuongezeka wa mapato haya ni kuimarishwa kwa Bandari
yetu kwa kuziba mianya ya ukwepaji kodi , kurekebishwa kwa misamaha ya
kodi ambayo hapo awali ilikuwa inachangia upotevu wa ukusanyaji wa
mapato, kuongezeka kwa matumizi ya utumiaji wa mashine za EFDs kwa
wafanyabiashara, Mamlaka kuwatengenezea mazingira mazuri kwa walipa
kodi, kudhibitiwa kwa eneo la forodha ambapo wajanja wachache walikuwa
wanatumia mwanya huu kuikosesha serikali mapato” amesema Kidata.
Kwa mwezi Januari walikusanya Trilioni 1,079,993.20:
Katika
kipindi cha Januari pekee, Mmalaka hiyo ilikusanya kiasi cha Trilioni
1,079,993.20 kwa Tanzania bara na visiwani ambapo kiasi hicho ni sawa
na Asilimia 102 ya lengo la Sh Trilioni 1,059,864.00 kwa mwezi.
“Makusanyo
haya ya Januari yametokana na ari na uthubutu ambao TRA imejiwekea
katika kusimamia na kuhakikisha inaendelea kuziba mianya ya Ukwepaji
kodi na kuweka mazingira rafiki kwa mlipakodi kwa kulipa kwa wakati na Urahisi kwa kutumia mifumo mbalimbali iliyopo”ameongeza.
Faini ya mashine za EFDs kwa Wafanyabaishara:
Kidata
amesema katika kipindi cha mwezi Februari pekee, Mamlaka hiyo
imefanikiwa kukusanya faini ya Sh 800milioni kwa watu wa jiji la Dar es
Salaam ambapo walikiuka na kufanya makosa katika utumiaji wa mashine
za EFDs.
“Kuanzia
mwezi Machi mwaka huu kila mtu anayetakiwa kutumia mashine za EFDs
atumie vinginevyo hatua kali za kisheria zitafuatwa”amesema Kidata.
Amesema
utaratibu wa matumizi ya EFDs ulifanyika kwa awamu mbili ambapo awamu
ya kwanza iliwahusisha wafanyabiashara ambao wamesajiliwa kutoa VAT na
awamu ya pili ilihusisha wafanyabaishara ambao hawakusajiliwa na Vat
ambao mauzo yao kwa mwaka ni zaidi ya Sh 14milioni.
Serikali kugawa bure mashine za EFDs:
Kwa
upande wake Kamishna wa Kodi za Ndani kutoka TRA, Yusuph Salum alisema
serikali imeagiza Mamlaka ya Mapato nchini kutoa bure mashine za EFDs
kwa wafanyabiashara wadogo ambao uwezo wa kununua mashine hizo unaweza
kuathiri mitaji yao ya biashara.
“Kwa
sasa tuko katika hatua za mwisho kukamilisha manunuzi wa mashine za
uniti 5700 na kwamba wafanyabiashara wakubwa hawatahusika na mgao wa
mashine hizi za bure bali wao wataendelea na utaratibu wa zamani wa
kujirejeshea gharama za mashine kupitia ritani za mwezi” amesema Salum.
Amesema
pamoja na kuwepo kwa sheria inayomtaka mfanyabiashara kununua , kutumia
mashine, kutoa risiti na kulipa kodi, TRA imebaini wafanyabiashara
waliowengi hawana mashine hizo za kutolea risiti pindi wanapofaya
mauzona hivyo kuikosesha serikali.
Usajili wa magari:
Kidata
alisema TRA, imefanya ukaguzi na kubaini kuwepo kwa magari ambayo
yaliingizwa nchini na kusajiliwa bila kufuata taratibu za forodha hivyo
kuyafanya yamilikiwe bila kulipiwa kodi stahiki na kwamba kuna jumla ya
magari 9000 Ambayo yanaingia nchini na kutolewa.
“Wamiliki
wa magari wote tayari tumeshawataarifu kufika TRA kufanyiwa uhakiki
ili kuyalipia kodi stahiki lakini pia kumekuwa na matumizi mabaya ya
misamaha iliyotolewa hasa kwa upande wa magari, hivyo utaratibu wa
misamaha uliwekwa kwa ajili ya kuwapa nafuu wawekezaji ili wahusika
wamekuwa wakiitumia vibaya kwani magari yameingizwa mengi kuliko
mahitaji na kupelekea serikali kukosa Mapato” amesema
Amesema
sheria za kodi zinatoa misamaha mbalimbali kupitia utaratibu wa Kituo Cha Uwekezaji cha Taifa(TIC) na mashirika yasiyo ya kiserikali na kwmaba
nia na Madhumuni ya misamaha hiyo ni kuvutia uwekezaji na kutoa unafuu
wa huduma kwa jamii.
Kufutwa kwa bei elekezi:
Katika
hatua nyingine, Mamlaka hiyo imefuta bei elekezi katika mchakato wa Uthaminishaji wa bidhaa bandarini kwa sababu ni kinyume cha sheria ya
Jumuiay ya Afrika Mashariki na kwamba TRA itaendesha shughuli za
kiforodha kulingana Na sheria husika.
“Tumeona
bei elekezi haisaidi kwa sababu uingizaji wa bidhaa unatawaliwa na Sheria ya Afrika Mashariki ambapo na sisi Tanzania ni wanachama, hivyo
Mamlaka itadhibiti ukaguzi na uthaminishaji halisi ili kila
mfanyabaishara alipe Ushuru na kodi kulingana na thamani ya bidhaa
husika, hata hivyo uthaminishaji Mizigo kwa wafanyabiashara umepelekea
wengine kulipa kodi kubwa kuliko Thamani ya bidhaa husika” amesema.
No comments:
Post a Comment