Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba
(kulia), akizungumza na wajumbe wapya wa kamati ya kitaifa ya matumizi
salama ya bioteknojia ya kisasa wakati akiizindua rasmi Dar es Salaam
leo katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI). Kushoto ni
Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Utafiti na Maendeleo, Hussein Mansour.
Msimamizi
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph
Ndunguru (kushoto), akitoa mada kuhusu zao la muhogo na changamoto za
magonjwa yanayolishambulia.
Baadhi ya wanakamati hao wakiwa ukumbini katika hafla
hiyo ya uzinduzi.
Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa bize wakati wa uzinduzi huo.
Wajumbe wa kamti hiyo
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mazingira, Dk. Julius Ningu
(kulia), akizungumza kwenye mkutano huo wa uzinduzi
Mkutano ukiendelea.
Waziri
Makmba (kulia), akiwaongoza viongozi wengine kutembelea maabara ya
kisasa ya utafiti ya MARI. Kutoka kushoto ni Msimamizi Mkuu wa Taasisi
ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph Ndunguru, Kaimu Mkurugenzi Utafiti na Maendeleo, Hussein Mansour na Profesa Raphael Chibunda.
Picha ya pamoja na Waziri Makamba.
Msimamizi
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph
Ndunguru (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri Makama na wajumbe wa
kamati Mpya jinsi maabara ya kisasa ya utafiti ya MARI inavyofanya kazi.
Mimea mbalimbali inayofanyiwa utafiti ikiwa katika chupa maalumu katika maabara hiyo.
Mbegu ya migomba iliyooteshwa baada ya kufanyiwa utafiti katika kituo hicho cha MARI.
Na Kalonga Kasati
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba
ameitaka kamati ya kitaifa ya matumizi salama ya bioteknojia ya kisasa
kutengeneza mpango kazi utakaosaidia kuharakisha shughuli zao na
kuisaidia serikali.
Makamba
alitoa mwito huo wakati akizindua kamati hiyo mpya katika Taasisi ya
Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI) jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
“Tengenezeni
mpango kazi wenu ili serikali iufahamu na kuweza kuwasaidia kifedha Endapo utakwama badala ya kukaa bila ya kuwa na dira na kusubiri kufanya Mikutano yenu ya kupitisha jambo fulani mara tatu katika kipindi cha
miaka nane” alisema Makamba.
Alisema
kamati hiyo ni ya muhimu sana katika utoaji wa maamuzi kuhusu masuala
ya Matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa na kukuza uelewa kwa
wajumbe wa kamati hiyo na wananchi kwa ujumla.
Alisema
Tanzania ni nchi mwanachama wa mkataba wa bioanuai wenye malengo Makuu
matatu, Hifadhi ya bioanuai, matumizi endelevu ya bioanuai na mgawanyo
sahihi wa faida zitokanazo na matumizi yake.
Alisema
Tanzania iliridhia mkataba huo mwezi Machi, 1996 ili kushirikiana na
Jumuia ya Kimataifa katika kutekeleza malengo yaliyotajwa.
Alisema
alisema changamoto kubwa ya teknolojia hiyo ya bioteknolojia ya kisasa Bado kuna wasiwasi kuhusu athari zinazoweza kutokea ambazo ni mzio,
kujitokeza kwa magugu sugu, saratani, usugu wa dawa kwa matibabu ya
magonjwa, wakulima kutegemea mbegu za kununua kila na madhara mengine
ambayo kwa sasa hayajawa bayana.
Msimamizi
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph
Ndunguru alisema wamejipanga kujenga kituo kikubwa cha utafiti kitakacho Gharimu dola za Marekani 556,000.
Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Hassan
Mshinda alisema ili wakulima waweze kufanikiwa katika kilimo chao ni
vizuri wakawa wanazingatia ushauri wa wataalamu ambao wamekuwa wakifanya Tafiti mbalimbali ambazo huwapelekea wao kwa matumizi ya kilimo.
No comments:
Post a Comment