Tuesday, 15 March 2016

Viongozi wa Chadema Arusha Warudi Ccm baada ya Uteuzi wa Katibu Mkuu

Viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha wameanza
kurudisha kadi za chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Mara tu baada ya uteuzi wa Katibu Mkuu mpya wa Chama.
 
Viongozi hao wa CHADEMA Arusha wametoa madai kadhaa ambayo yamewafanya kufikia uamuzi huo kwa nyakati tofauti.
 
Mwenyekiti wa Mtaa wa Olumuriaki Ndugu Godfrey Kitomari na wanachama wanachama wa
Chadema 97 wa Kata ya Sombetini wamerudi CCM kwa sababu zifuatazo;-

1. Kuridhishwa na kasi ya Mhe Dkt Magufuli.
 
2. Kuchukizwa na Mbowe kukiuza chama na kuiacha agenda ya kukemea ufisadi kama ilivyokuwa Mwanzo na badala yake kuwatetea.
3. Uteuzi wa Katibu Mkuu asiye na uwezo lakini mwenye rekodi mbaya kwenye jamii.
[​IMG]
Pichani: Ndugu Kitomari akiveshwa Kofia ya CCM kwenye Mkutano wa hadhara wa kukaribishwa CCM.
[​IMG]
Wananchi wa Kata ya Sombetini wakishuhudia tukio la Mwenyekiti huyo wa Mtaa kujiunga na CCM.
[​IMG]
WanaCCM wakimlaki Ndugu Kitomari mara baada ya kujiunga na Chama hicho.
Katika tukio jingine; 
Mwenyekiti wa BAVICHA Kata ya Mjini Kati Ndugu Ally Kaole (pichani) naye
amejiuzulu nafasi yake hiyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi – CCM.

Kaole ametoa sababu za uamuzi wake huo kuwa ni;-
1.
Uteuzi wa Katibu asiyekijua Chama lakini asiyejua falsafa za Uongozi na
Utawala, amesema uteuzi huo unalenga kuua Chama hicho. Ndugu Ally
amedai kuwa Katibu Mkuu mpya wa CHADEMA na yule aliyestaafu hawafanani
hata chembe, ni sawa na kufananisha Kifo na Usingizi.

2.
Amesikitishwa na Mwenyekiti wa Chama kutetea majipu tena hadharani,
akisema hatua hiyo imeondoa uhalali wa yeye kuwepo katika chama hicho
ambacho aliamini kuwa kinachukizwa na majipu na kwamba kilikuwa kinaomba
ridhaa ili kuyashughulikia.

[​IMG]
Pichani: Ndugu Ally Kaole (aliyekuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Arusha.

No comments:

Post a Comment