Na Chripino Mpinge
Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM) umekanusha tuhuma zilizotolewa na baadhi ya
wafanyakazi waendeshaji wa chuo hicho kwenye baadhi ya vyombo vya habari
kuwa unaendesha vitendo vya dhuluma, uonevu na upendeleleo katika
ulipaji wa mishahara na kuwasahau watumishi hao jambo linalokwamisha
ufanisi wa chuo hicho.
Taarifa ya kanusho dhidi ya
tuhuma hizo iliyotolewa na Ofisi ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Dar es salaam, Utawala na kusainiwa na Prof.Preksedis Marco Ndomba leo
jijini Dar es salaam imeeleza kuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam
kinaendeshwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia
Utumishi Umma nchini na kamwe hakina mamlaka ya kumwonea, kumdhulumu
wala kutoa upendeleo kwa mtumishi yeyote kwa kuwa suala hilo liko nje ya
misingi iliyoanzisha chuo hicho.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kama
ilivyo kwa vyuo vingine vya umma suala la maslahi hasa nyongeza za
mishahara na marupurupu mengine ya watumishi wa vyuo hususan Chuo Kikuu
cha Dar es salaam linapangwa na kuidhinishwa na Serikali kupitia Ofisi
ya Msajili wa Hazina na siyo uongozi wa chuo hicho.
Aidha, mishahara ya watumishi
wa chuo hicho hupangwa kulingana na kanuni na taratibu za Serikali na
kuongeza kuwa wanataaluma wa Chuo hicho hupewa mishahara yao kutokana na
Muundo wa Pamoja wa Utumishi wa Wanataaluma wa Vyuo Vikuu vya Umma wa
mwaka 2014 na Sheria ya Kazi na mahusiano kazini ya mwaka 2004 na Kanuni
za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009.
Kuhusu tuhuma za kuwepo kwa
tofauti ya mishahara miongoni mwa watumishi wa Chuo hicho imeeleza kuwa
hilo inatokana na tofauti ya vyeo waliyonayo watumishi hao na kuongeza
kuwa wao kama viongozi wa chuo hicho hawana mamlaka ya kuwapangia
mishahara watumishi wala kutengeneza nyaraka za mishahara.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa
Chuo Kikuu cha Dar es salaam hupokea nyaraka za mishahara kwa watumishi
kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina na kuzitekeleza na kuwataka watumishi
hao kutambua kuwa tofauti ya vyeo waliyo nayo inawafanya walipwe
mishahara tofauti.
Kupitia taarifa hiyo uongozi wa
chuo hicho umeeleza kuwa hakuna upendeleo katika nafasi za uongozi
chuoni hapo kwa kuwa nafasi zote hujazwa kwa kufuata hati idhini ya
chuo, pia hupatikana kwa kushindanishwa kwa waombaji kwa sifa zao na
inapotokea mtumishi katika nafasi ya Mkurugenzi uendeshaji anastaafu
kazi Menejimenti ya chuo humwomba mwanataaluma kutoka chuoni hapo
kukaimu nafasi hiyo wakati taratibu za kuitangaza nafasi hiyo ili
kumpata mkurugenzi mpya zikiwa zinaendelea.
Kwa upande wa tuhuma ya kuwepo
kwa matumizi mabaya ya mali za chuo hasa magari kwa safari zisizohusiana
na chuo hicho imefafanua kuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kina Sera,
Kanuni na miongozo mbalimbali inayodhibiti matumizi ya magari na mali za
umma ikiwemo ujazaji wa vitabu maalum vya makabidhiano ya magari ” Log
Book”.
Taarifa imebainisha kuwa UDSM
hudhibiti matumizi ya magari yake kwa kuyawekea maandishi ubavuni na
kwamba magari hutakiwa kuegesha chuoni baada ya matumizi saa 12 jioni
na wafanyakazi wanaoyatumia kinyume na miongozo iliyowekwa wanachukuliwa
hatua za kinidhamu.
Aidha, ili kuboresha maslahi ya
watumishi wa chuo hicho hasa upandishwaji wa vyeo ndani ya chuo muundo
wa Utumishi wa wafanyakazi waendeshaji hutumika pia maboresho hufanyika
kupitia vikao rasmi vya ajira kulingana na matakwa ya sheria ya kazi.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa
Menejimenti ya chuo hicho baada ya kubaini kuwepo kwa changamoto
zilizojitokeza katika utekelezaji wa muundo wa Utumishi wa Waendeshaji
iliamua kuuhuisha na kuuwasilisha kwa Msajili wa Hazina ili ufanyiwe
kazi.
Pia kikao cha Baraza la Chuo
Kikuu cha Dar es salaam kilichofanyika Februari 12, 2016 pamoja na mambo
mengine kilielekeza Chama cha Wafanyakazi UDSM kwa kushirikiana na
Uongozi wa chuo kuandika muhtasari unaoaininisha changamoto za watumishi
zilizopo ili ziwasilishwe katika Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini atembelea masoko.
Mbunge wa jimbo la Moshi
mjini,Jafary Michael akisalimiana na wafanyabiashara wa soko la Pasua
alipofanya ziara ya kutembelea masoko yaliyopo katika mji wa Moshi
kusikiliza kero za wafanyabiashara hao.
Mbunge wa jimbo la Moshi
mjini,Jafary Michael akiongozana na Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi
,Raymond Mboya wakitembelea soko la Mbuyuni kusikiliza kero mbalimbali
pamoja na kuona namna bra ya kuboresha masoko hayo.
Mbunge wa jimbo la Moshi
mjini,Jafary Michael akiongozana na Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi
,Raymond Mboya wakitembelea soko la Mbuyuni kusikiliza kero mbalimbali
pamoja na kuona namna bra ya kuboresha masoko hayo.
Mbunge wa jimbo la Moshi
mjini,Jafary Michael akiongozana na Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi
,Raymond Mboya wakitembelea soko la Mbuyuni kusikiliza kero mbalimbali
pamoja na kuona namna bra ya kuboresha masoko hayo.
Mbunge wa jimbo la Moshi
mjini,Jafary Michael akiongozana na Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi
,Raymond Mboya wakitembelea soko la Majengo kusikiliza kero mbalimbali
pamoja na kuona namna bra ya kuboresha masoko hayo.
No comments:
Post a Comment