Tuesday, 15 March 2016

Ujumbe wa Jwtz Watembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania WashIngton

New Picture (9)kutoka kushoto: Col. Adolph Mutta (DA), Brig. Gen. (Dkt) Denis R. Janga, Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi, Brig. Gen. (Dkt) Robinson M. Mwanjela, Lt. Col. (Dkt) Charles E. Mwanziva na Lt. Col. Lawerence T. Banda.
……
Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC alikutana na Ujumbe wa JWTZ ulioongozwa na Mkuu wa Tiba Jeshini, Brigedia Jenerali (Dkt.) Denis Raphael Janga, aliyekuwa amefuatana na Mkuu wa Chuo cha Kikeshi cha Tiba – Lugalo, Brigedia Jenerali (Dkt) Robinson Mboni Mwanjela. Wengine ni Mkurugenzi wa Kinga Jeshini, Luteni Kanali Charles Emilio Mwanziva pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wauguzi, Luteni Kanali Lawrence Tia Banda. Ujumbe huo ulikwa na ziara ya Kikazi ya wiki moja hapa Marekani, katika kuendeleza mahusiano baina na JWTZ na majeshi ya Marekani.

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI MHANDISI MASAUNI AMPOKEA WAZIRI MKUU NA KUTEMBELEA KAMBI YA MWISA

1Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kushoto), akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa alipotembelea Kambi ya Utenganisho ya Mwisa,iliyoko wilayani Misenyi,mkoani Kagera, kambi hiyo inahifadhi wakimbizi waliotengwa kutoka katika makambi ya wakimbizi kutoka nchini Burundi kwa sababu za kiusalama.
2Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa(kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya wakimbizi,iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke. Waziri Mkuu alitembelea Kambi ya Utenganisho ya Mwisa,iliyoko wilayani Misenyi,mkoani Kagera, kambi hiyo inahifadhi wakimbizi waliotengwa kutoka katika makambi ya wakimbizi kutoka nchini Burundi kwa sababu za kiusalama.
3Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa(kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya wakimbizi,iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Selemani Mziray. Waziri Mkuu alitembelea Kambi ya Utenganisho ya Mwisa,iliyoko wilayani Misenyi,mkoani Kagera, kambi hiyo inahifadhi wakimbizi waliotengwa kutoka katika makambi ya wakimbizi kutoka nchini Burundi kwa sababu za kiusalama.
4Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa,akizungumza na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani), wakati alipotembelea kambi ya Utenganisho ya Mwisa iliyoko wilayani Misenyi, mkoani Kagera. kambi hiyo inahifadhi wakimbizi waliotengwa kutoka katika makambi ya wakimbizi kutoka nchini Burundi kwa sababu za kiusalama.Katikati Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Mwigulu Nchemba na kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.
5Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kushoto), akimuongoza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa(wa pili kulia) kwenda kuongea na wakimbizi waliohifadhiwa katika kambi ya Mwisa,iliyoko wilayani Misenyi,mkoani Kagera.Anayefuatia baada ya Waziri Mkuu ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja na wa mwisho ni Mkuu wa Magereza mkoa wa Kagera, SACP Omari Mtiga

No comments:

Post a Comment