Wednesday, 9 March 2016

Rais Dkt John Pombe Magufuli Amempokea Rais wa Vietnam Mhe Truong Tang Sang

K1Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang akiwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi na wafanyakazi wa Ikulu mara Baada ya kuwasili.
K2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang wakati walipokuwa wanazungumza Ikulu jijini Dar es Salaam.
K3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Mazungumzo Rasmi kati ya ujumbe wa Tanzania na Ujumbe wa Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang Ikulu jijini Dar es Salaam
K4Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuzungumza na wanahabari hawapo pichani Ikulu jijini Dar es Salaam.
K5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari hawapo pichani kuhusu mazungumzo yao na Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang Ikulu jijini Dar es Salaam.
K6Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni Wake Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang Ikulu jijini Dar es Salaam.

Serikali kuunda Mamlaka Kuu ya Mapato ya Taifa

KADA
Kaimu Kamishna wa TRA Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari(Hawapo pichani) katika mkutano wa kuota taarifa juu ya ukusanyaji wa kodi kwa mwezi Februari.

Na Chrispino Mpinge

Serikali ipo kwenye mpango wa kuunda Mamlaka ya Mapato Kuu ya Taifa nje ya Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) iliyopo kwa sasa ili kuondokana na malalamiko ya kero za kodi kwa wananchi wenye kipato cha chini.

Hayo yamesemwa leo Jijini  Dar es Salaam na Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Alphayo Kidata alipokuwa  akifafanua kuhusu juhudi za Serikali katika kuwasaidia Wananchi wa kipato cha chini kuweza kumudu kulipa kiwango cha kodi kinachowekwa na na Mamlaka hiyo.

“ Napenda kuwambia umma wa watanzania kwamba Serikali ya Awamu ya tano inawajali watu Wake na ndio maana imeona kuwa kuna haja ya kuunda  Mamlaka moja ya utozaji wa kodi itakayojumuisha taasisi zote zinazohusika na kukusanya mapato nje ya kodi na ushuru ili kuondokana na malalamiko mengi ya wananchi juu ya utozaji wa kodi hasa katika Halmashauri zetu”Alisema Kidata.

Kamishna Kidata amesema kuwa katika dunia hii hakuna Serikali ambayo imechaguliwa na Wananchi ikaamua tu kuwakandamiza wananchi wake katika jambo lolote lile hivyo basi kwa Sasaserikali ipo  katika mchakato wa kuunda Mamlaka hiyo ambayo itasaidia kuweka viwango vya kodi ambavyo wananchi wa hali ya chini watamudu kulipa kutokana na biashara au kazi wanazozifanya.

Kamishna huyo ameongeza kuwa Mamlaka yake kwa kushirikiana na mamlaka nyingine Zinazokusanya kodi katika Halmashauri nchini watahakikisha wanalipatia ufumbuzi suala la kero Ya kodi kwa wananchi wa hali ya chini kwa kupata muafaka ambao utasaidia pande zote mbili bila kukandamiza upande wowote iwe Serikali ama mwananchi wa kawaida.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuwa na rekodi nzuri ya ukusanyaji wa kodi ila kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kodi ambazo zimekuwa kero na Hazina tija. Hivyo Serikali imejipanga kuiongezea nguvu Mamlaka hiyo kwa kuipa uwezo wa kukusanya na mapato ambayo  hayatokani na kodi toka katika wizara, mashirika,tasisi za serikalina Halmashauri zote nchini.

Maombi Maalum YaKumwombe Rais Dkt John Pombe Magufuli  Na Serikali Yake  Yafanyika Jijini Mbeya

Baadhi ya maaskofu kutoka makanisa mbalimbali Mkoani Mbeya wakiwa wamshika Picha ya Rais  na ramani ya Tanzania wakati wa maombi maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya.
Picha ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ikiwa imeshikwa na maaskofu wa makanisa mbalimbali Mkoani Mbeya kwa ajili ya kufanya maombi maalumu kwa ajili ya rais na serikali yake katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya
Muongozaji Mkuu wa Maombi ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli ,Askofu Dkt  Charles Gadi wa kanisa la The City of refuge Church  yenye makao makuu jijini Dar es salaam akizungumza na waumini walioshiriki katika maombi hayo katika ukumbi wa Mkapa .
Askofu Dkt  Charles Gadi wa kanisa la The City of refuge Church  yenye makao makuu jijini Dar es salaam akizungumza na waumini walioshiriki katika maombi ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake  katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya March 8 mwaka huu. .
Baadhi ya waumini walioshiriki Maombi Maalum ya Kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake yaliyoandaliwa na Jukwaa la wakristo Mkoani Mbeya kwa kushirikiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la The City of refuge Church Dkt Charles Gadi katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya March 8 mwaka huu.
Baadhi ya maaskofu  na waumini kutoka jukwaa la Wakristo Mkoa wa Mbeya wakiwa katika maombi maalumu ya kumwombea Rais Dkt  John Pombe Magufuli na serikali yake katika ukumbi wa Mkapa jijni Mbeya Machi 8 mwaka huu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali mkoani humo.
kwaya zikiendelea kutumbuiza katika maombi hayo ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya Machi 8 mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa  kushoto pamoja na Askofu Charles Gadi mwenye miwani  wakiwa katika maombi maalum ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Maombi yakiendelea….
Baadhi ya viongozi wa makanisa mbalimbali mkoani mbeya wakiwa katika maombi maalumu ya kumwombea Rais Dkt Maguli na serikali yake .

No comments:

Post a Comment