MABONDIA Mada Maugo na Abdallah
Pazi ‘Mfalme wa waalamu’ wamendelea kutambiana kwa ajili ya mpambano
wao utakaofanyika siku ya March 27 sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa
ndani wa Taifa
akizungumza wakati wa kutambulisha mpambano wao uho
Bondia Mada Maugo amesema kuwa
Pazi i mtoto mdogo sana katika ulimwengu wa masumbwi Nchini hivyo
inambidi afanye mazoezi ya kutosha ili avuke japo raundi ya nne mana
sitakuwa na msalia mtume wakati wa kupambana
Pia naomba mashabiki zangu
wafike mapema kwa ajili yakuona ninavyomsambalatisha Pazi mapema mana
nimewapa bonanzi ya raundi nne mashabiki zangu
Akijibu mapigo hayo bondia Pazi
amesema yeye kwa sasa ndio anatamba nchini hivyo yeye ni Mfalme na akuna
wa kuusambalatisha ufalme wake kwani kilicho mkuta bondia aliempiga
China kwa K.o ya raundi ya tatu ndicho kitakacho mkuta yeye kwani kesha
zeeka sasa ni wakati wa damu changa pekee
Nae mratibu wa mpambano uho
Rajabu Mhamila ‘Super D’ amesema mbali y mpambano uho Unaosubiliwa kwa
hamu na mashabiki lukuku kutakuwa na mipambano ya kukata na shoka
Ambapo bondia Nassibu Ramadhani
atakumbana na Fansic Miyeyusho na bingwa wa mikanda Miwili ya Afrika
U.B.O na WPBF, Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ atkumbana na Deo Samweli
Na Pius Kazaula atakumbana na Seba Temba mpambano mwingine utawakutanisha Cosmas Cheka na Mohamed Matumla
Katika mpambano uho kutakuwa
na uhuzwaji wa vifaa vya mchezo wa ngumi pamoja na DVD za Mafunzo ya
mchezo wa ngumi kwa ajili ya kutambua sheria mbalimbali za mchezo
zitakazokuwa zikitolewa bule kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo
na vingine kuuzwa kwa galama nafuu
No comments:
Post a Comment