Friday, 4 March 2016

Kongamano la Moyo wa Mwanamke kufanyika Kanisa la Living Water Centre Kawe

Katika kuelekea siku ya mwanamke Duniani Kanisa la Living Water Centre Kawe kupitia huduma ya Wamama kanisani
Hapo ikiongozwa na mmbeba maono Mwalimu Lilian Ndegi wameandaa Kongamano linalojulikana kama “Kongamano la Moyo Wanawake”
 Kongamano hilo huwa linalofanyika mara moja kila mwaka Katika Kanisa la Living Water Centre Kawe chini ya mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi na Mwalimu Lilian Ndegi,Kongamano hili ni kwa kusudi la kuwajenga Wanawake kuwa na uwezo Katika kumtumika Mungu na kujua nafasi yao ya kutumika aliyowapa katika ufalme Mungu.
Theme ya mwaka huu ni Mwanamke Mjenzi Mithali 14:1 Kusudi kuu la Kongamano ni Kuwafanya Wanawake kuwa watendaji
katika ufalme wa Mungu na wawajibikaji na watekelezaji wa majukumu katika ngazi ya Familia,Huduma,Jamii na Taifa kwa ujumla.
Waimbaji Women of The Kingdom,Living Waters,More than Enough Band na wengine wengi.
Karibuni sana.Mawasiliano 0713 580 400 

CITY IKO MORO,KUIVAA SIMBA JUMAPILI

city1 city2Kikosi cha Mbeya City Fc  kimewasili salama  mkoani Morogoro tayari kwa kambi ya Muda  kujindaa na mchezo wa ligi kuu ya Soka  Tanzania  Bara dhidi ya Simba Sports Club  uliopangwa kuchezwa  Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa jjini Dar es Salaam.

Akizungumza na mbeyacityfc.com mapema leo asubuhi kocha Msaidizi wa City, Mohamed Kijuso Amesema  kikosi kimewasili salama na leo watafanya mazoezi ya Jioni kwenye Uwanja wa Chuo Cha Jordan kilichopo mkoani hapa yatakayofatiwaa na program maalumu ambazo zitakuwaa Zikiongozwa na Mwalimu Kinnah Phiri  kabla ya kuivaa Simba Siku ya jumapili jijini Dar.

“Tutakuwa Uwanjani Jumapili dhidi ya Simba  kwenye uwanja wa Taifa,hilo ndiyo jambo kubwa Naweza kusema, tumesafiri na kufika hapa Morogoro hali za wachezaji wote 18 zikiwa  salama, kwa hilo Tunamshukuru Mungu,jioni ya leo Tutafanya Mazoezi  hapo chuoni Jordan na kesho Tutakuwa na program Maalumu amabazo Mwalimu ameziandaa” alisema.

Kuhusu Simba, Kocha huyo kijana ameweka wazi kuwa timu hiyo kutoka Mtaa wa Msimbazi ni Nzuri hivyo Hawataibeza hata kidogo licha ya matatizo kadhaa yaliyopo kwenye kambi yake kwa Sasa, na kusema kikosi chake kitaingia Uwanjani kupambana kwa Nguvu zote kuhakikisha City inaibuka na Ushindi.

“Nafahamu Simba wana matatizo madogo kwenye kambi yao hivi sasa,jambo hilo halitufanyi kuwabeza, Bado ni Timu nzuri na iko kwenye nafasi ya juu kwenye Msimamo wa ligi tofauti na sisi, Tutaingia Uwanjani kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha Tunaibuka  na ushindi ili tuweze kujiimarisha zaidi, hivi sasa tunahitaji Matokeo kwenye kila mchezo jambo ambalo pekee litatutoa Tulipo na kutupeleka sehemu nyingine alisema”.

Akiendelea zaidi Kijuso alisema kuwa, anafahamu Simba ina wachezaji wengi vijana na wenye kasi Pia inatumia Nguvu nyingi kumiliki mpira kwenye eneo la kiungo hivyo  ni wazi City itatumia kikosi Tofauti na kile kilichozoeleka huku mbinu  za kuhakikisha wanaziba nafasi zote  kwenye eneo la katikati ya uwanja zikiwa tayari zimeshafanyia kazi.

No comments:

Post a Comment