Monday, 14 March 2016

Jamii imetakiwa kuhakikisha Vifo Vitokanavyo na Matatizo ya Uzazi kwa akina Mama Wajawazito na Watoto Nchini

1 
Na Mwandishi Wetu

Jamii imetakiwa kuhakikisha vifo vitokanavyo na matatizo ya uzazi kwa akina mama wajawazito na watoto nchini vinatokomezwa
 
Hayo yamesemwa leo na katibu mkuu wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya alipotembelea zahanati ya kijiji cha uturo kilichopo wilayani Mbarali Ambacho wananchi wa kijiji hicho wanashiriki moja kwa moja katika kuondoa matatizo hayo
 
Dkt.Mpoki alisema serikali katika kutekeleza sera ya afya nchini inahakikisha akina mama wajawazito na watoto wachanga hawafi kwa magonjwa yanayozuilika
 
“Gharama za afya zimekuwa Kubwa sana,hivyo nguvu yetu na umoja ndiyo njia pekee ya kujikomboa na kuleta maendeleo ya nchi na kutokomeza vifo vya akina mama nchi nzima”alisema
Aidha,aliwataka wananchi kujua afya ni wajibu wa kila mtu na inawezekana endapo kila mtu Atajitolea kuhakikisha huduma za kiafya zikiwemo za kliniki na tabia ya kuzalia nyumbani Zinaachwa.
 
Hatahivyo katibu mkuu huyo aliitaka mikoa mingine kufika kijijini hapo kujifunza ni jinsi gani Wamefanikiwa kuwashirikisha wananchi wote hususan akina baba kushiriki kuanzia ujauzito hadi mtoto anapozaliwa
 
Naye Mkuu wa Zahati hiyo Tabibu  Wilson Chotamganga alisema kijiji hicho kimefanikiwa kutokomeza vifo hivyo kwa kuunda kuunda timu ya viongozi wa Vitongoji wa huduma za uzazi na Mtoto pamoja na kuanzisha madaftari mawili ya mama wajawazito na watoto chini ya miaka Mitano na kukubaliana sheria Ndogodogo za kutozwa shilingi elfu tano kwa yeyote atakayekiuka Makubaliana na taratibu zilizowekwa.

No comments:

Post a Comment