Saturday, 12 March 2016

Ccm yataka wakurugenzi wa manispaa ya Ilala Wawajibishwe kuchelewesha Uchaguzi wa Meya Jijini Dar es salaam

Na Kalonga Kasati

CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam kimemuomba Waziri Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene kuwawajibisha Wakurugenzi wa Manispaa ya Ilala na Kinondoni kwa kile walichodai ni kuvuruga uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.

Hayo yalizungumzwa Dar es Salaam jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar e Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’ wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kumekuwa na sintofahamu hadi sasa kuhusiana na uchaguzi huo kutokana na woga wa wakurugenzi hao ambao wameshindwa kujiamini.
” Wakurugenzi hawa ndiyo chanzo cha vurugu katika uchaguzi huu wa meya tumewaomba wakurugenzi hawa watoe tamko na tafsri sahihi ya ushiriki kwa wajumbe wenye sifa ili kuacha kuupotosha umma juu ya uchaguzi huu,”alisema Gadafi.
Gadafi alisema kuwa wakurugenzi hao kwa makusudi na huku wakifahamu wanakiuka sheria waliruhusu baadhi ya maswahiba wao kutoka chama cha upinzani ( Ukawa) ambao walitoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam kuingia kwenye uchaguzi uliovurugika.
Gadafi alisema mwanachama yeyote wa CCM anaruhusiwa kufanya uchaguzi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kupingwa kama taratibu unavyoelekeza.
Alisema hizi kauli zinazotolewa kuwa haiwezekani wajumbe wakatoka nje ya Dar es Salaam na kupiga kula eneo lingine hazina ukweli wowote kwani siku za nyuma ziliwahi kufanyika kwa vyama vingine lakini hakukuwa na kulalamika.

Aidha katika hatua nyingine Simba amesema Meya wa Ukawa walioshinda katika Manispaa za Kinondoni na Ilala wanatakiwa watambue kuwa Halmshauri hizo hazitaendeshwa kwa ilani ya chama chao bali ni ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa asilimia 60 ya bajeti ya maendeleo inaongozwa na chama. 

INAFRIKA BAND AKA “WAZEE WA INDEGE” KUTUMBUIZA MAREKANI (FESTIVAL OF NATIONS)

7e6c7f86-d634-4da9-af7d-b83958f68951
Na Tabu Mullah
Bendi maarufu Inafrika band aka Wazee wa Indege wanatarajiwa kuruka wakati wowote ule kuelekea nchini marekani kushiriki katika maoyesho makubwa ya kimataifa ya Festival of nations ,yatakayo fanyika katika Dollywood Theme Park,bendi hii kutoka Tanzania ndio bendi pekee iliyoteuliwa kuliwakilisha bara la Afrika katika maonyesho hayo ya kimataifa.
Inafrika band itakuwepo nchini marekani katika ziara ya kikazi kwa muda wa miezi mitatu kuzikonga nyoyo za washabiki wa kimataifa nchini marekani.
Kuchaguliwa kwa Inafrika band kushiriki maonyesho hayo makubwa kunatokana na mvuto wa muziki wa bendi hiyo kukubalika zaidi kimataifa.
Muziki ambao una maadili ya kitanzania ambako nje ya mipaka umewateka
washabiki wengi wa kimataifa.  
Bendi hiyo yenye makao jiji Dar-es-salaam imejikuta haina muda wa kupumzika kutoka na wingi Tour za kimataifa kwa muda wa miaka 10 sasa.
Ni kama wiki mbili tu bendi hiyo imerudi kutoka safari ya nchi 19 za bara la ulaya. Tunawatakia kila la heri Inafrika Band aka Wazee wa Indege katika kutuwakilisha huko Marekani. Bendi hiyo ilikuwapo Dollywood ,Marekani mwaka 2014 na kuwanasa washabiki wengi  na muziki wao wa kitanzania

No comments:

Post a Comment