Makamu
Mwenyekiti wa kikao cha bodi ya barabara Mkoa wa Pwani Ridhiwani
Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze akifafanua jambo
katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa
wa Pwani.
Mbunge
wa viti maalumu Mkoa wa Pwani kushoto Zainabu Vulu akiwa na wajumbe
wengine waliohudhuria katika kikao hicho, wa kati kati ni Mwenyekiti wa
halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamisi Dikupatile.
Meneja
wa wakala wa barabara Tanroad Mkoa wa Pwani Tumaini Salakikye akitolea
ufafanuai na kujibu maswali yalioulizwa na wajumbe wa kikao hicho juu ya
miundombinu ya barabara.
Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akichangia hoja katika kikao hicho cha bodi ya barabara.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya mji wa Kibaha Leornad Mlowe akitolea ufafanuzi
kuhusiana na kero ya ubovu wa barabara katika Wilaya ya Kibaha.
Na Kalonga Kasati
IMEELEZWA kwamba kutokana na
mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali Hapa nchini
zimeweza kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara na
madaraja katika baadhi ya maeneo ya mkoani Pwani hali ambayo imekuwa ni
kero kubwa kwa wananchi kutokana na magari kukwama hivyo kutokupitika
kwa urahisi.
Hayo yamesemwa na Mhandisi
mkuu wa kitengo cha mipango kutoka Wakala wa barabara Tanroad Mkoa wa
Pwani Zuhura Amani wakati akiwakilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi
za Matengenezo na miradi ya maendeleo kwa wajumbe wa kikao cha bodi ya
barabara cha Mkoa, Ambapo amesema kuwa kuharibika kwa miundombinu hiyo
kunarudisha nyuma jitihada za serikai katika kuleta huduma kwa jamii.
Zuhura alisema kuwa jumla ya
kiasi cha shilingi bilioni 20.9 zilipangwa kutumika kwa ajili ya Matengenezo ya barabara kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2014 hadi 2015
lakini kutokana na kuwepo kwa ufinyu wa bajeti zoezi hilo halikuweza
kufanikiwa kwa wakati uliopangwa.
Kwa upande wao wajumbe
waliohudhuria katika kikao hicho akiwemo Mwenyekiti wa CCM katika
Wilaya ya Kibaha Mji,Maulid Bundala pamoja na Katibu msaidizi wa Mkoa
wa Pwani Shangwe Twamala walisema hai hiyo ya ubovu wa barabara
inachangia kwa kiasi kikubwa kukwama kwa magari hivyo kupelekea usumnufu
mkubwa hasa katika kipindi cha mvua.
Nao baadhi wa wabunge wa Mkoa
wa Pwani akiwemo Ridhiwani Kikwete Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambaye
ndio alikuwa makamu Mwenyekiti katika kikao hicho alisema kwamba baadhi
ya maeneo ya barabara kwa sasa zipo katika hali mbaya ktokana na
nyingine kupita kwake ni vigumu kutokana na kuwa na mashimo mengi.
“Kwa hii kwa kweli Meneja na
timu yako inabidi kuliangalia kwa macho matatu kwani kuna Baadhi ya
barabara nyingine katika Mkoa wetu wa Pwani zipo katika hai mbaya sana
maana Wakati mwingine nashindwa kuelewa tatizo ni nini kwa suala hili
naomba mfanya jitihada za kufanya ukarabati ili barabara zetu ziweze
kupitaka kwa urais,”alisema Ridhione.
Kwa upande wake Mbunge wa
Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa alisema kwamba katika Jimbo lake kuna
barabara ni muhimu sana ya kutoka Nyamwage kulelekea Utete ambapo ndipo Makao makuu wa Wilaya hiyo inahitajika ifanyiwe matengenezo ili iweze
kupitika kwa Urahisi.
“Asilimia 19 la pato la Taifa
inategemea katika Wilaya ya Rufiji kutokana na misitu iiyopo hivyo
kunahitajika juhudi za makusudi kabisa kuhakikisha barabara ambazo ni
kiunganishi kikubwa Zifanyiwe ukarabati na zingine ziwekwe katika
kiwango cha lami ili kuweza kuleta chachu ya maenedlea kwa wananchi wa
rufiji na Taifa zima kwa ujumla,” alisema Mchengerwa.
Akijibu malalamiko hayo Meneja
wa wakala wa barabara Tanroad Mkoa wa Pwani Tumaini Salakikye amekiri
kuwepo kwa hali hiyo na kuongeza kwamba changamoto kubwa inayowakabili
katika utekelezaji wa majukumu yao ni kutokana na bajeti kuwa ndogo.
Barabara zenye kiwango cha
changarawe na udongo katika baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Pwani kwa
sasa zimeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo
mbali mbali hivyo kunahitajika nguvu ya makusudi kutoka serikalini ili
ziweze kufanyiwa matengenezo ya haraka.
No comments:
Post a Comment