Naibu Waziri Wa Afya Hamis Kigwangala
Waziri wa afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee Na Watoto Ummy Mwalimu Amefanya Ziara ya Ghafla katika hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Na kukutana na Dosari Mbalimbali
Moja ya mambo yaliyomkera Ummy ni kuwakosa Madaktari wa Zamu katika Hospitali hiyo pamoja Na ukosefu wa Mashuka kwa Wagonjwa Hali iliyowalazimu kutandika kanga zao.
Ilikuwa ni ziara ya kustukiza iliyofanywa na Waziri wa afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia wazee Na watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga ikiwemo Ukosefu wa vitanda pamoja na Madaktari Walioajiriwa kutokuwepo.
Mwalimu anatembelea Vitengo Mbalimbali vya Hospitali Hiyo na kukutana madaktari Wanafunzi Huku wale Madaktari Waajiriwa Walioko Zamu Wakiwa hawajulikani walipo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga ,Ambaye aliambatana na Ummy Mwalimu Dk.Marcel Clemence alisema Madaktari Waliokuwa Zamu Wamefanya Makosa kuwaachia Hospitali Madaktari Wanaojifunza Hivyo lazima Watawajibishwa.
Ziara ya Ummy Mwalimu imekuja Baada ya kuwepo kwa Malalamiko ya kauli Chafu Zilizokuwa zikidaiwa kutolewa na Wauguzi kwa Wagonjwa Hususani katika Wodi ya Wazazi.
No comments:
Post a Comment