. Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na
Manyara na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla (aliyesimama)
akizungumza na wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya
Arusha, Kilimanjaro na Manyara (hawapo pichani) ambazo Zimeamua kufanya
kazi kwa pamoja ili kudhibiti Utoroshaji wa Madini ya Tanzanite nje ya
nchi. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini,
Mhandisi Omar Chambo, wa kwanza kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Manyara,
Eliakim Maswi na wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud
Ntibenda.Chambo Akizungumza na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara wakati wa Mkutano huo.Afisa
Madini Mkazi katika Ofisi ya Madini Mirelani, Mhandisi Henry Mditi
akitoa taarifa ya kazi zinazofanywa na Ofisi hiyo iliyopo katika wilaya
ya Simanjiro Mkoani Manyara. Wanaosikiliza ni Katibu Mkuu Wizara ya
Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa pili kushoto), Wa kwanza
kushoto ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje. Wengine
katika picha ni Kamishna Msaidizi wa Madini sehemu ya Uthaminishaji
Madini, Latifa Mtoro (wa kwanza kulia) na wa Pili kulia ni Mkurugenzi wa
Taasisi ya Uunganishaji na Ushirikishi Wadau katika Tasnia ya Uziduaji
(EISF), Catherine Lyombe.
Na Teresia Mhagama na Asteria Muhozya
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo
ameeleza kuwa madini Aina ya Tanzanite Yaliyokamatwa yakitoroshwa Nje ya
nchi Bila kuwa na Vibali Tarehe 15 Desemba, 2015 kupitia Uwanja wa
ndege wa Kilimanjaro (KIA) yamefikia Thamani ya Dola za Marekani milioni
1,207,990.
Katibu Mkuu alisema hayo jijini Arusha wakati Wa kikao chake na
Kamati za Ulinzi na Usalama Za Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara Ambazo Zimeamua kufanya kazi kwa pamoja ili kudhibiti Utoroshaji wa
madini ya Tanzanite na kufuatilia kwa karibu shughuli za uchimbaji na Biashara ya Madini hayo ili yanufaishe Taifa.
Katibu Mkuu alisema kuwa Tanzanite hiyo Ghafi Yenye Uzito wa Gramu
2,015.59 ilikuwa ikitoroshwa na Raia wa India, Jain Anurag Aliyekuwa
akitaka kuelekea Mji wa Jaipur kwa kutumia Shirika la ndege la Qatar.
“Nataka niwaeleze Watanzania wanaoshirikiana na Raia wa kigeni
kutorosha Tanzanite kuwa Wajiepushe na Biashara hii Haramu kwani hatua
kali zitaendelea kuchukuliwa Dhidi yao na hatuna Mzaha katika hili,”
alisema Mhandisi Chambo.
Alieleza kuwa Madini hayo yaliyokamatwa Yameshataifishwa kama ambavyo
sheria na kanuni Za Madini Zinavyoelekeza na kwamba Zoezi hilo la Ukamataji watorosha madini Hufanywa na Wizara ya Nishati na Madini
kupitia Wakala wake wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) kwa kushirikina na
Taasisi nyingine kama Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Jeshi la Polisi,
Idara ya Usalama wa Taifa, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Idara ya
Uhamiaji.
Aidha alieleza kuwa Serikali itafuta leseni za Wafanyabiashara wa Madini Watakaobainika kutorosha Rasilimali Hiyo nje ya nchi ikiwemo
kuwakamata Wachimbaji na WafanyaBiashara Wanaokwepa kulipa kodi stahiki
kwa Serikali.
“Ili kudhibiti Utoroshaji Madini Unaofanywa na WafanyaBiashara Wenye
leseni na wasio na leseni, Wazawa na Wasio Wazawa, Tumeshajipanga kwa
kushirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa Mitatu ya Manyara,
Kilimanjaro na Arusha ili kudhibiti Hali hii na Tanzania ibaki kama
kinara katika Uzalishaji na Uuzaji wa Madini haya na sio Nchi nyingine,” Alisema Mhandisi Chambo.
Kuhusu Wachimbaji Wadogo nchini, alisema kuwa Serikali itaendelea
kugawa Maeneo ya uchimbaji Madini kwa wachimbaji hao ikiwa ni pamoja na Utoaji Ruzuku, Uagizaji wa zana kama baruti na Utoaji wa Mafunzo Huku
akitoa angalizo kuwa Wachimbaji Hao Wanapaswa kuwa Waaminifu na
kuhakikisha kuwa Wanalipa kodi Stahiki Serikalini Badala ya kusubiri
kuchukuliwa hatua za kisheria.
Wakati Huohuo Mwenyekiti wa Kamati za Ulinzi Na Usalama za mikoa ya
Arusha, Kilimanjaro na Manyara na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos
Makalla ametoa masaa 24 kwa Raia wa kigeni wote Wanaojihusisha na Biashara ya Madini ya Tanzanite na Madini Mengine kinyume Cha sheria
kuondoka Nchini Mara Moja na Watakaokaidi agizo hilo Watachukuliwa Hatua
kali za kisheria.
Agizo hilo alilitoa Baada ya Kamati Hiyo kubaini kwamba Uwepo wa Wageni Mbalimbali kutoka nje ya nchi hususani Kenya, Sri Lanka, Nepal na
India Ambao Hujihusisha na Biashara ya Tanzanite bila kuwa na leseni Zinazowaruhusu kufanya hivyo na Hatimaye Hutorosha Madini hayo kwenda
nje ya Nchi.
“Madini Haya Yanauzwa kama Njugu Hivyo Tumeona kwamba Sisi Kamati za
Ulinzi na Usalama za mikoa Hii Mitatu Tukishirikiana kuimarisha ulinzi Tutakomesha Suala hili, Tunataka kuona Watu Wanaouza Madini ni wale
wenye leseni tu, na Wachimbaji na Wafanyabiashara Wahakikishe Wanalipa
kodi stahiki kwani kuanzia Tarehe Tano Januari operesheni ya kuwakamata
itaanza,” alisema Makalla.
Vilevile alieleza kuwa wafanyakazi wa kigeni Waliopo katika Mgodi wa
Tanzanite One Unaomilikuwa na kampuni ya Sky Associates kwa kushirikiana
na Serikali ambao Hawana Vibali vya kufanya kazi na Wale Wenye Vibali
vya kufanya kazi ambazo Zingeweza kufanywa na Watanzania Waondoke Mgodini hapo.
“Mchango wa Madini katika Pato la Taifa bado Hauridhishi na sisi Tunafanya kila Jitihada ili Tanzanite hii ambayo inachimbwa Tanzania
peke Yake ifaidishe nchi, kila Mwananchi anao Wajibu wa kuhakikisha hili
linafanikiwa, Wadau wa Madini Wana Wajibu wa kuhakikisha kwamba Wanalipa kodi Stahiki na kutoa taarifa za hujuma Zozote Zinazofanyika Ambazo Baadhi ya wazawa Wanashirikiana na Wageni kuiibia nchi Rasilimali Hii Muhimu,” alisema Makalla.
No comments:
Post a Comment