Shughuli ikiendelea ya kutoa Elimu kuhusiana Na Mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa Elimu kwa Madereva kutokutumia Simu na kilevi wakati wote Wakitumia vyombo vya Moto.Kampeni hiyo inaendeshwa na Jeshi la polisi la Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.
Na Mwandishi Wetu
Kampeni ya Usalama Barabarani ya kuwataka Madereva Nchini kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani,leo imefanyika
katika Mkoa wa Dodoma.
Madereva Wameendelea kuhimizwa kutotumia Vinywaji vyenye Ulevi na kuacha Tabia ya kuongea na Simu au kutuma na
kupokea ujumbe wa Maneno (sms) Wanapokuwa Wanaendesha vyombo vya Moto.
Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa
wa Dodoma, SSP Nuru Selemani amesema kampeni Hii ni muhimu katika
kupunguza Matukio ya Ajali “Watumiaji wa Barabara hii ya Mkoa wa Dodoma Ni Wengi Hususani Madereva Wa vyombo vya Moto Hawana Budi kuzingatia Maelekezo Ambavyo Tumekuwa Tukiwapa katika kampeni hizi ili Tupate Matokeo Mazuri kwa kupunguza Ajali kama ilivyokusudiwa”Alisema
Alisema Madereva Wakizingatia Sheria za Barabarani kwa kiasi kikubwa Ajali Zinazoendelea kutokea kila Siku
zitapungua Hususani katika kipindi hiki cha Msimu Unakoelekea wa Sikukuu
na Aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuunga mkono jitihada za Serikali
katika kupambana na Tatizo Hili ambalo limekuwa Sugu .
Kwa upande wake,Kaimu Mkuu wa kanda ya kati
wa asoko wa Vodacom Tanzania Heladius Kisiwani, alisema Vodacom
itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuunga mkono Jitihada za
kuondoa Matatizo kwenye Jamii kama lilivyo tatizo hili la ajali ili
kuhakikisha wananchi Wanaishi Maisha Murua na Marefu.”Tunatoa rai kwa Madereva Wote kuzingatia Sheria za Barabarani na kutokutumia simu Wakati
wowote Wakiwa Wanatumia Vyombo vya Moto”.
Aliongeza kuwa Vodacom itakuwa mstari wa
mbele kuelimisha jamii athari za kuendesha gari wakati huo huo unatumia
simu ya mkononi kupitia kampeni ya “Wait to Send” pia itaendelea
kuhamasisha madereva kuzingatia Sheria za usalama barabarani.
Alisema kampuni hiyo itaendeleza kutoa Elimu kwa Mikoa mingine pia katika Uhamasishaji wa madereva kuzingatia
sheria za barabarani katika miji ya Morogoro,Dar es Salaam na mikoa
mingine na kampeni hizi zitaendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini.
Katika kampeni ya leo Wafanyakazi wa
Vodacom kwa kushirikiana na Askari wa Usalama Barabarani Walitoa Uhamasishaji kwa Madereva kuacha kuongea na Simu Wanapoendesha vyombo
vya Moto na kuwagawia Madereva pete maalum Za kuwatahadharisha kutotuma Ujumbe wa Simu Za Mkononi Wanapokuwa Wanaendesha vyombo vya Moto pia Zoezi la kupima Madereva kubaini kama Wanatumia vilevi lilifanyika Ambapo Madereva Waliokutwa Wanaendesha Vyombo vya Moto Walichukuliwa Hatua kali za kisheria.
Baadhi ya Abiria Walioshuhudia kampeni hii Mkoani Dodoma Wamesema ni ya Muhimu itasaidia kupunguza Ajali Nchini.”Hivi sasa ajali Nyingi Zinazotokea Hapa Nchini Zinasababishwa Na Uzembe wa Madereva,kampeni Hizi Zikiendelea Zitapunguza Ajali kwa kiasi
kikubwa”.Alisema Sunday Israel Mkazi wa Dodoma Aliyekuwa Safarini
kuelekea Singida.
No comments:
Post a Comment